GET /api/v0.1/hansard/entries/988633/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 988633,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/988633/?format=api",
"text_counter": 211,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Nilikuwa ninasema ya kwamba ni ukweli kwamba saa zingine vile ambavyo majina ya watu yanaharibiwa ndio huleta shida katika familia. Utaona ya kwamba haswa Kilifi imetajwa sana katika mambo haya ya COVID-19. Katika Kilifi, kuna naibu wa gavana ambaye alitajwa. Bw. Saburi ana mke na watoto watatu. Wale watoto watatu na mke wake walifanyiwa vipimo na hakuna hata mmoja alipatikana na virusi hivyo. Yeye pia ako na stakabadhi za hospitali za Kenyatta National Hospital, Nairobi Hospital na Mombasa Hospital. Vipimo hivyo vyote vilionyesha kwamba hana virusi hivyo. Tabia kama hiyo ni ya kuharibia watu majina. Hivi sasa mtu kama Bw. Saburi hawezi kutembea mahali popote hapa Kenya. Inavunja heshima ya familia na inaweza pia kutenganisha familia. Ni lazima kuwe na heshima. Hususan ikiwa jambo liko kortini, ni vibaya sana kwa mtu kama Rais kusema kwamba huyo mtu afungwe miaka kumi. Ni aibu na makosa kwa Rais kumtaja Bw. Saburi. Kwa hivyo, heshima si utumwa. Sio vizuri kusema kwamba katika Kilifi kuna watu ambao wako hivi na vile. Hivi sasa idadi ya maambukizi katika Kaunti ya Kilifi iko chini kuliko kaunti zingine. Kwa hivyo, heshima ni lazima idumishwe. Hivi sasa heshima ya mtu kama naibu gavana ndani ya nyumba yake, watoto wake, jamii yake na marafiki zake imeharibika sana. Lazima kuwe na uchunguzi na heshima idumishwe katika mambo haya ya COVID-19. Asante, Bw. Naibu Spika."
}