GET /api/v0.1/hansard/entries/990006/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 990006,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/990006/?format=api",
"text_counter": 44,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "kwa sababu walikuwa wameona kwamba malalamishi yao yamewezwa kutekelezwa. Mhe. Spika, matatizo yako katika mabunge ya kaunti na vile vile yako katika ofisi ya Auditor kwa sababu ile miradi yetu gushi ambayo imefanyika ama imedaiwa kufanyika, haingii katika ripoti ya Auditor. Kwa hivyo, ikiwa haikuandikwa katika ripoti ya Auditor, hakutakuwa na swali ambalo litaulizwa na Auditor kwa mfano: Kwa nini barabara hii ilikuwa inatakikana itengenezwe na haikutengenezwa? Mhe. Spika, ofisi ya Contoller of Budget pia inahusika katika mambo kama haya kwa sababu wao ndio wanajuwa pesa ngapi zimetolewa na ni kwa miradi gani. Kwa hivyo, mwisho wa mwaka, ile miradi gushi zote ambazo zimetengenezwa na pesa zikaliwa, hakuna hata moja inayotokea katika ripoti ya Auditor . Kwa hivyo, hii ni njia ambayo imepangwa mahususi ya kuweza kula pesa za kaunti. Hii ni kwa sababu hakuna njia ambayo unaweza kujua mpaka uwe unaishi katika eneo lile ambalo unaweza kuenda mwenyewe ukathibitisha kwamba ule mradi haukufanyika. Kwa hivyo, Bw. Spika, ile Kamati husika ambayo itapewa Petition hii ni lazima isafiri Narok ili iweze kuthibitisha kwamba hii miradi ni gushi na wale wahusika wote wakamatwe na washtakiwe. Asante."
}