GET /api/v0.1/hansard/entries/990322/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 990322,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/990322/?format=api",
"text_counter": 360,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika. Kwanza, ninamshukuru ndugu yangu Sen. Sakaja kwa kuleta jambo hili. Cha muhimu zaidi ni kwamba kukitokea shida kama ile niliyoiona katika sehemu fulani ya Nairobi ambayo ameitaja, ni jambo la kusikitisha kuona watoto wachanga, akina mama na vijana wakihangaika sana. Niliona kama ni kitendo cha unyama ambacho hakijatendeka katika taifa hili; kuona mama na mtoto wakitupwa kando bila kujali kilicho ndani ya nyumba. Mali inatupwa na kuvunjwa. Hata sufuria ambazo pengine wangeweza kupikia baada ya hiyo ghasia, nazo pia zinatupwa. Hao Wakenya wenzetu ambao hata kama wameketi kwenya ardhi ambayo si yao, si vizuri kufurushwa kama kwamba hawalindwi na sheria zetu. Kuna wakati inatakikana tuweke sura ya ubinadamu katika utendakazi wetu, hasa polisi ama kukiwa kuna amri ya kwenda kuvunja makao fulani. Inatakikana tuone ya kwamba hata ikiwa hayo yatafanyika, watoto, akina mama na vijana wadogo wanaokwenda skuli hawataathirika. Ni picha mbaya kuona vitabu vyao vikiloa maji na kutapakaa kila pahali. Wakati mwingine mbinu zao za kujikimu zinaharibiwa na hata wakitolewa kwenye makao hayo hawateweza kuendelea na maisha yao. Waswahili walisema kwamba mwenzako akinyolewa, nawe tia kichwa chako maji. Nilikuwa katika lili hili Bunge na Sen. Sakaja akiwa hapa na nikasema kwamba maeneo ya Mtwapa watu wanavunjiwa nyumba, wanateswa sana na kutupwa nje; mali inatupwa pande zote kwa sababu ya bwanyenye mmoja aliyedai kuwa ardhi hiyo ni yake. Baadaye mnakuja kujua kwamba hiyo hati miliki aliyonayo ni bandia. Wale watu waliofurushwa, watafanywa namna gani na yeye alikuwa na amri ya kortini? Ubinadamu ni kitu muhimu sana na Serikali ni lazima iangalie. Wakati huu wa COVID-19 ni mbaya. Sio wakati wa kuchukua hatua kama hii. Huu si ugonjwa wa kucheka. Kila mtu ulimwengu mzima anauogopa. Ni jambo la kuzingatia sana kama Wakenya. Si kuwadharau Wakenya wenzetu kwa sababu wameketi mahali na kuwatoa kwa sababu tuna uwezo. Lazima Serikali ikomeshe mambo kama haya kwa wakati huu na iangalie mambo ya ugonjwa kwanza. Bw. Spika, la mwisho ni kwamba, wale watu wakati huu wanahitaji dawa na chakula. Wanaishi hapa Nairobi na ni Wakenya. Ni wagonjwa, wanalala barabarani, kwenye misitu na maeneo ambayo hayafai binadamu ama mnyama yeyote kulala. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}