GET /api/v0.1/hansard/entries/990380/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 990380,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/990380/?format=api",
    "text_counter": 418,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": ". Lakini, genge la majambazi walivamia yadi ya Mombasa Maize Millers usiku wakavunja magari, wakaiba mali, wote wakisimamiwa na polisi katika Kaunti ya Nakuru. Bw. Spika, hii inamaanisha kwamba tuna Serikali ya kihuni. Hatuna Serikali ambayo inaheshimu sheria na utengamano. Waziri wa Afya anasema kwamba tuondoe kutanagamana kwa sababu ya COVID-19, lakini wale wanaofurushwa Kariobangi, wanasongamana. Polisi wanaokuja kufurusha watu hatujui kama wana COVID-19 ama hawana. Wao wanatangamana na watu katika maeneo ambayo hakuna njia yeyote ambayo tunaweza kuwatengenisha. Bw. Spika, nchi yetu imekuwa sasa ni mtu mwenye nguvu afanye vile anavyotaka kwa sababu unaeza kutoa watu usiku wa manane bila sababu yeyote. Ardhi na stakabadhi zinaonyesha kwamba anayemiliki ama aliye pale yuko pale kihalali. Kwa hivyo, ni lazima kama Seneti, tukemee swala hili kwa sababu ni jukumu letu kuhakiksha kwamba Serikali inatekeleza mambo kulingana na sheria. Kwa hivyo, ikiwa Serikali yenyewe ndio inavunja sheria, ina maana kwamba nchi yetu inakwenda mkondo ambao si sawa. Asante kwa kunipa fursa hii."
}