GET /api/v0.1/hansard/entries/991723/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 991723,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/991723/?format=api",
"text_counter": 28,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Wa Spika. Pia nawapa kongole wale ambao wameleta Ombi hili kutoka Kaunti ya Machakos. Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba haki za wafanyikazi zinakandamizwa sana katika serikali za kaunti. Nilifanya kazi katika korti ya kuangalila masilahi ya wafanyikazi hapa Kenya, mfanyikazi aliye chini haheshimiwi. Ni muhimu kila mtu humu nchini aheshimiwe katika utenda kazi wake. Lazima kila mikono miwili inayofanya kazi iregeshewe asante kulingana na haki, mshahara na kazi iliyotendwa. Katika hili Ombi, tunaona kwamba hawa walifanya kazi na hawakusema kwamba wanataka kuondoka, wala hatujui ni kwa sababu gani waliachishwa hiyo kazi."
}