GET /api/v0.1/hansard/entries/992885/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 992885,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/992885/?format=api",
    "text_counter": 161,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bi Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Jambo la kwanza nampatia kongole Seneta shupavu na mkongwe wa kisheria na aliyekuwa mwenyekiti wangu katika muungano wetu wa wanasheria katika Kenya. Ndugu yangu anawakilisha eneo la huku Nyamira, Sen. Omogeni. Nilikuwa najiuliza kama ana jina la kizungu. Tulikuwa tunajadiliana hapa na dada yangu Sen. (Dr.) Musuruve na tukaona kwamba Sen. Omogeni hana jina la kizungu. Yeye anaitwa Sen. Okong’o Omogeni. Ninamshukuru sana kwa kukubali kuchukua kesi hii na kuifanya yeye bila malipo kutoka kwa PSC au kwetu sisi Maseneta kuchanga kwa minajili ya kutaka kumlipa yeye kama wakili. Aliweza kujitolea mhanga, akatumia akili zake na taaluma na hatimaye ameleta mazao ndani ya Seneti. Kongole ndugu yangu kwa kazi yako njema. Bi. Spika wa Muda, tukiwa hapa, mara nyingi tumeona ya kwamba wengine wanependa uamuzi unaofanywa ndani ya korti na wengine hawapendelei. Lakini, mimi kama mwanasheria nasema kwamba sheria ni kama panga, inakata pande mbili. Wewe unaweza kupenda ama usipenda, lakini sheria ni kama panga na inakata pande zote mbili. Ni lazima ikate katikati, kusema ya kwamba huu ndio ukweli na huu si ukweli. Hii ndio njia sawa na hii si njia sawa. Kwa hivyo, sisi sote tunakubaliana na ule uamulizi uliotolewa na Korti yetu ya juu zaidi kuliko korti zote katika Kenya, yaani Supreme Court . Uamuzi huo ulilingana sana na taratibu za wale waliokaa pale, wakaangalia na wakaona kwamba kuna umuhimu kuwa na Bunge la Seneti katika Kenya. Bi. Spika wa Muda, la muhimu ni kwamba uamuzi huu umeleta bayana kati ya Bunge la Kitaifa na Bunge la Seneti ili tuweze kufanya kazi pamoja bila kukosana. Sisi kama Maseneta tunafuata Kipengele 96 Cha Katiba ya Kenya, kinachosema kwamba jukumu kuu la Seneti na kila Seneta ni kutetea serikali za kaunti. Jukumu lingine nikuangalia ugavi wa pesa. Juhumu hii ni muhimu na uti wa mgongo wa serikali zetu za ugatuzi. Kuna umuhimu wa watu kukaa na kuelewana. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}