GET /api/v0.1/hansard/entries/993060/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 993060,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/993060/?format=api",
"text_counter": 31,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Shukrani, Bw. Spika. Kwanza, ningependa kukupa kongole kwa uamuzi wako ambao wazungu wanauita Solomonic wisdom juu ya vile tunaweza kufanya kazi wakati huu mgumu katika Bunge la Seneti. Madhumuni ya Kanuni za Bunge la Seneti ni kusaidia utaratibu wa kuendesha kazi ama majadiliano katika Bunge na vile Maseneta wanaweza kupiga kura kuambatana na mfumo wa delegations. Wakati huu ni mgumu sana katika historia ya nchi yetu na ulimwengu mzima kwa jumla. Tunaambiwa ugonjwa kama huu ulitokea zamani kabla sisi kuzaliwa. Hivi sasa, hili janga la COVID-19 ni janga ambalo hakuna mtu yeyote aliyelitarajia kubuika. Kukabiliana na huu ugonjwa una taratibu zake ambazo zimepeanwa na shirika la ulimwengu linaloshugulika na afya. Shirika hilo ni World Health Organization (WHO). Taratibu kama hizo zemepeanwa na Serikali yetu ikiongozwa na Wizara ya Afya. Taratibu hizi ni jinsi watu wanaweza kujipanga ile waepukane na huu ugonjwa na vile tunaweza kukabiliana nao. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}