GET /api/v0.1/hansard/entries/993066/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 993066,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/993066/?format=api",
"text_counter": 37,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Nataka kuungana na wenzangu kupongeza uamuzi wako ambao ni wa busara. Hii kwa sababu janga la COVID-19 liko nasi na ni lazima tukubali kukumbatia teknolojia. Teknolojia ndio itatusaidia wakati huu mguu wa kuendelea na maisha yetu. Nimemsikiliza Sen. Mutula Kilonzo Jnr. akisema kwamba ni vizuri tutafute sehemu ambayo Maseneta wote wanaweza kutoshea. Nilimsikiliza kwa makini nikaona ni kama anaongea mambo mawili kwa wakati mmoja. Alisema kwamba tukumbatie teknolojia na pia tutafute sehemu ambayo Maseneta wote wanaweza kutoshea. Ni vizuri kukumbatia teknolojia kwa sababu tuko na ujuzi na vyombo ambavyo vinahitajika. Ni vizuri janga hili liwe kama funzo kwetu. Tusiseme kwamba baada ya janga hili kutuondokea tutarudi pale pale tulikotoka. Liwe kama funzo kwetu ili tukumbatie teknolojia kama mataifa mengine ya ulimwengu ambayo yameendelea. Sisi tuna uwezo na ujuzi wa kufanya hivyo. Bw. Spika, ningependa kukubaliana na wewe vile ulivyosema mia kwa mia. Tutaendelea na mikutano yetu tukitumia vyombo vya teknilojia."
}