GET /api/v0.1/hansard/entries/993486/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 993486,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/993486/?format=api",
"text_counter": 290,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Sen. (Prof.) Kindiki ni rafiki, ndugu na shemeji yangu. Yeye amesoma vitabu mpaka akafika kiwango cha Profesa. Lakini kwa upande wa siasa, nafikiria alinoga. Lakini hayo yakijiri, mimi nataka kusema kwamba kuna mwanafalsafa mmoja aliyeishi zamani na alikua msomi, Niccolò Machiavelli. Mimi nmekua nikisema kila siku kwamba ikiwa wewe umechaguliwa au umeandikwa kazi, usiwe mwerevu kuliko bosi wako. Machiavelli alisema hayo katika mambo ya utawala na madaraka. Dhana hii inajulikana kama Principles of Power. Unaweza kuwa umesoma sana kama Sen. (Prof.) Kindiki na pengine bosi wake hakufika kiwango cha elimu kama hiyo, lakini si sababu ya kutumia akili yako wakati bosi amekwambia ufanye hivi au vile halafu unafanya kinyume. Mimi natoka katika chama cha Orange Democratic Movement (ODM) na ni lazima niheshimu Mhe. Raila Amolo Odinga. Jambo la pili nikukiheshimu chama changu. Vile chama changu kinanielekeza, ni lazima niangalie na nifuate mkondo wake. Nikikosa kufuata mkondo--- Basi ni kama ninataka kuachana na hicho chama na nitafute njia ya kwenda. Kule nitakapokwenda sijui kama ni kuzuri ama ni kubaya. Kuna msemo kwamba unaweza kuacha kuzuri ukifikiria kule kwingine ndiko kizuri zaidi, ukakuta ndiko kubaya zaidi kuliko kule ulikotoka."
}