GET /api/v0.1/hansard/entries/993516/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 993516,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/993516/?format=api",
"text_counter": 320,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipatia fursa hii kuchangia Mswada wa Kiranja wa upande wa wengi katika Bunge la Seneti. Kabla sijatoa maoni yangu, ningependa kumsahihisha ndugu yangu, Sen. Madzayo, aliposema kwamba Sen. (Prof.) Kindiki katika siasa alinoga. Nafikiria lengo lake lilikuwa kusema kwamba ‘alilamba lolo’. Kunoga ni kufanya vizuri zaidi kuliko vile ambavyo inatarajiwa. Niko hapa kwanza kusema kwamba ndugu yetu, Sen. (Prof.) Kindiki, ni mtu mwenye tajriba kubwa. Ni mtu ambaye alifanya kazi yake kama Naibu wa Spika kwa uzoefu mwingi na vile vile kwa hekima kubwa. Maamuzi aliyofanya ni ya kuaminika na yameweza kutumika hata katika mahakama za nchi yetu ya Kenya. Bw. Spika, sisi sote katika Bunge hili, mbali na wale wachache ambao wamekuja kama wabunge huru, tunadhaminiwa na vyama vya kisiasa. Leo siasa inaweza kukubali na kesho ikakukataa. Kwa hivyo, Hoja hii haina shaka kwamba lengo hapa ni la kisiasa sio la kuangalia kazi ya Sen. (Prof.) Kindiki ilikuwa namna gani katika Bunge la Seneti. Lazima tumpatie faraja ndugu yetu, Sen. (Prof.) Kindiki, ya kwamba ameweza kufanya kazi vizuri na sasa imefika wakati wa kurudi na awe kama sisi Maseneta wengine ambao tunahudumu na mwisho wa siku tunakwenda kwetu na watu wetu wanafurahia kazi zetu. Nina hakika Sen. (Prof.) Kindiki atakuwa mtu mwenye kutupatia msaada mkubwa katika majadialiano ambayo yataendelea katika Bunge hili kuliko vile alivyokuwa katika kiti cha Naibu wa Spika. Bw. Spika, chama kikikosa imani na wewe, sisi kama Maseneta katika Bunge hili hatuna njia nyingine ya kuepukana na swala kama hilo. Vyama ndivyo vinatudhamini. Chama kikiwa hakina imani ina maana kwamba muda wako wa kuhudumu katika nyadhifa ambayo umepewa na chama umeisha hata kama ulichaguliwa kwa kura katika Bunge hili. Ningependa kuwakosoa wale ambao wamezungumza mbeleni na kusema kwamba maamuzi yamefanywa mahali pengine. Ni kweli hata wakati wa uchaguzi wa Bw. Spika, Naibu wake na wenyeviti wa kamati mbali mbali ulipofanywa mara ya kwanza, uliamuliwa mahali pengine. Kuna ndugu zetu walikuwa kupiga kura upande wetu lakini wakasema uamuzi umefanya, kwa hivyo sisi hatuwezi kuenda kinyume na uamuzi ule. Bw. Spika, hili sio jambo la kwanza. Kuenda mbele, siku za usoni kutoka mwanzo tukatae maamuzi yanayoamuliwa sehemu ambayo sisi Maseneta hatuko. Tukikataa kufanyiwa kwa maamuzi mahali pengine ndio tutaweza kuipatia Seneti hii nguvu ya kusimama mahali popote na kutetea haki ya mwananchi wa kawaida. Bila The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}