GET /api/v0.1/hansard/entries/993577/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 993577,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/993577/?format=api",
"text_counter": 381,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "heko, unasema unamtimua. Huko ndiko ninasema ni kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa, na yeye mwenyewe lazima ajue Kiswahili. Kwa Sen. Sakaja, nitakuwa nimekosea kuja hapa kuzungumza kwa lugha ya Kiswahili ambayo yeye haielewi wala haimanyi. Mimi sina uwezo wa kumsaidia bali ninamwambia sisi tunazungumza kwa lugha ambayo wenzangu wa kutoka pengine Pwani wanaifahamu. Ningependa kumwambia Naibu wa Spika, Sen. (Prof.) Kindiki, kwamba Biblia yangu inaniambia hata ijapokuwa unapitia katika bonde la mauti, usiogope kwa sababu Mwenyezi Mungu yuko pamoja nawe. Vile vile napenda nikwambie kwamba kama vile Yesu alivyokuwa amebebeshwa msalaba, kwa sababu naona ndugu yangu unaelekezwa Golgotha, naona taharuki imetanda na ninaona hawa ndugu zangu watakuelekeza Golgotha. Mimi, Sen. Kinyua, nitakubebesha msalaba kama vile Yesu alivyobebeshwa na Simon wa Kirene. Nitasimama kama Simon wa Kirene nikubebeshe kwa sababu akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki. Nitakusaidia kwa sababu hata nawe umekuwa na sisi na umetembea na sisi. Ndugu zangu nawaomba kwamba mtu akifanya kazi nzuri, apewe hongera. Hawa ndugu zangu wa mrengo huu wa Wachache Bungeni, leo wanatuambia vile tunavyopaswa kujua uaminifu kwa chama. Unawezaje kujua uaminifu wa Chama cha Jubilee ilhali wewe uko katika Chama cha Orange Democratic Movement (ODM)? Ni kosa kuja kutufunza mambo ya uaminifu. Sen. (Prof.) Kindiki ni mwaminifu; amekuwa na ataendelea kuwa mwaminifu. Utajuaje uaminifu wa chama cha Jubilee ilhali wewe uko katika chama cha Orange Democratic Movement (ODM)? Itakuwa kosa ninyi kutufunza uaminifu. Sen. (Prof.) Kindiki ni mwaminifu na amekuwa mwaminifu na ataaendelea kuwa mwaminifu. Bw. Spika, nitamueleza Sen. (Prof.) Kindiki tutakuwa marafiki wa kufa kuzikana. Asante sana."
}