GET /api/v0.1/hansard/entries/993774/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 993774,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/993774/?format=api",
    "text_counter": 80,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Ninakubaliana mia kwa mia kwamba kilimo ndio uti wa mgongo na pia ninawashukuru ndugu zangu, Sen. Khaniri na Sen. Cherargei, kwa kuleta Taarifa hii hapa. Itakuwa jambo la aibu kuona kwamba mwaka nenda mwaka rudi, nchi yetu inakumbwa na janga la njaa. Kila siku kila uchao, tukilala na tukiamka, tunaagiza chakula kutoka nje ilihali nchini yetu inajulikana kama nchi ya ukulima. Tunavyoelewa ni kwamba, ni kweli kabisa nchi yetu ni ya ukulima lakini Serikali lazima iwajibike kuona kwamba wanachukua mazao kutoka kwa wakulima na kuweka katika maghala. Vile vile, Serikali pia isaidie wakulima kwa njia mbali mbali ili wafaulu katika hiyo biashara ya mazao. Bi. Spika wa Muda, mara nyingi, watu wamekuwa wakisema inabidi tulete mahindi ya rangi ya njano na nyeupe kutoka Mexico na Brazil. Tunaambiwa pia mahindi hayo yana ugonjwa. Sasa ni wakati gani Serikali yetu itawajibika kuona mkulima wa mahindi, majani chai au kahawa, anapata faida kutoka kwa mazao yake? Tumeelimishwa kuhusu mazao ya shamba na tumeona kwa sasa, ni ufisadi mtupu ambao unaendelea. Maghala yetu yote ya National Cereals and Produce Board (NCPB) hayana kitu kwa sasa. Ndio sababu tunapata taabu. Hata Serikali ikijaribu kupeana chakula kwa watu wasiojiweza ama hawaweza kutoka nyumbani, hasa wakati huu wa janga la COVID-19, inakuwa ni vigumu. Kuna maeneo fulani ambayo yamezingirwa na hakuna ruhusa ya kutoka. Kwa mfano, Old Town kuna wazee na vijana wanaolalamika, kwa sababu, wanataka nafasi ya kujiangalia katika maisha yao. Utakubaliana nami kwamba kuna ufisadi katika ugavi wa chakula hiki ambacho hata hakitoshi. Hivi sasa pesa nyingi zimepatikana kusaidia Kenya kununua chakula na kuona kwamba wananchi wanaishi vyema. Hata kama hizi pesa ni za janga la COVID- 19, utasikia pia kuna ufisadi na watu wanaiba. Lazima Serikali ichukue hatua mwafaka ya kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wanaofanya ufisadi ili wajitetee huko mahakamani. Bi. Spika wa Muda, mimi ninatoka Kaunti ya Kilifi ambako tunategemea uchumi kutoka kwa mazao ya shamba. Eneo kama Magarini linajullikana sana kwa maembe matamu kuliko Malindi na sehemu zingine hapa Kenya. Vilevile, eneo Bunge la Magarini liko na mananasi matamu zaidi lakini wakulima wa mananasi na maembe hawapati msaada wowote kutoka kwa Serikali. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}