GET /api/v0.1/hansard/entries/993830/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 993830,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/993830/?format=api",
    "text_counter": 136,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "huyu halipwi Hardship Allowance na wanafanya juu chini kuhakikisha kwamba, watoto wetu wanasoma vizuri. Kwa nini walimu hawa wanabaguliwa katika nchi yetu? Kwa nini hawapati marupurupu yao kuambatana na kanuni za TSC? Katika kaunti yangu ya Kwale, ndipo pabaya zaidi hata afadhali kwako wewe Kitui. Kuna walimu karibu 25 wameleta ombi kwangu kulalamikia tatizo kama lili hili. Wengine wamekuwa naibu walimu wakuu karibu miaka kumi na marupurupu ya hardship hawapati. Posho ya ugumu hawapati, ilhali kazi wanazofanya ni kubwa sana kuhahakikisha watoto wetu wanapata elimu. Kwa hivyo, ninaunga mkono Taarifa hii. Taarifa hii itakapoenda katika Kamati ya Elimu, ninatumaini kwamba, watakaa chini na kutafuta njia kwa haraka sana kuhakikisha kwamba, hawa walimu ambao Taarifa yetu imesoma hapa waweze kupandishwa daraja mpaka kule juu. Asante sana. Ninaunga Taarifa hii mkono."
}