GET /api/v0.1/hansard/entries/993929/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 993929,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/993929/?format=api",
    "text_counter": 23,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "Asante sana, Bi Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii kuchangia Taarifa hii ambayo imesomwa na Seneta jirani, kwa sababu Kwale na Mombasa ni kaunti jirani. Kusema kweli, hali ya uchumi na biashara katika Kaunti ya Mombasa imekuwa mbaya sana. Tegemeo kubwa kabisa la watu wa Pwani ni bandari. Ikiwa mizigo haitachukuliwa na magari pale bandarini, italeta shida kubwa sana. Kwa hivyo, ninaonelea kwamba lazima kupatikane njia mwafaka. Tunapaswa kujua tutafanya nini ili kila mtu mwenye biashara aweze kupata riziki yake. Kuna hali ngumu ilioko katika nchi yetu. Ugonjwa wa COVID-19 isiwe sababu ya wasafirishaji kutoweza kupakia mizigo yao au kufanya biashara. Bi Spika wa Muda, kwa hivyo, ninaunga mkono Taarifa hii ya Seneta wa Kaunti ya Mombasa. Tuhakikishe kwamba Waziri wa Uchukuzi anaulizwa kwa nini hii sheria inaendelea namna hii. Ni lazima watu wafanye kazi na kupata riziki yao. Asante sana."
}