GET /api/v0.1/hansard/entries/993935/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 993935,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/993935/?format=api",
"text_counter": 29,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili kuchangia Taarifa hii ambayo ilimeletwa hapa na Sen. Faki. Taarifa hii inahusu usafirishaji wa mizigo kutoka Mombasa hadi sehemu zingine nchini kwa kutumia Standard Gauge Railway (SGR) na malori. Mwaka uliopita, viongozi wa Mombasa walikutana na Katibu Mkuu na wakakubaliana juu ya usafirishaji wa mizigo kutoka bandari ya Momabasa. Walikubaliana kuwa katika soko huru ni vizuri waache malori na SGR zibebe mizigo kulingana na vile wanabiashara wataamua. Nashangaa kuona wakati huu Katibu Mkuu anatumia COVID-19 ili kuleta Mswada huo. Hii ni kinyume na makubaliano yalikuwa kati ya viongozi na Katibu Mkuu. Ni vizuri viongozi kuheshimiana kwa sababu tunawakilisha wananchi wetu. Makatibu Wakuu pia wanafanya kazi kwa niaba ya wananchi. Tulisema ya kwamba uchumi wa Pwani na maeneo mengi ambayo malori yanapitia umeathirika sana. Kisa na maana ni kwamba Serikali iliamua kutumia SGR kubebe mizigo yote. Ikiwa utasafiri kutoka Mombasa, Mariakani, Samburu, Mackinnon Road, Voi na Mtitio Andei utaona jinsi wananchi wengi wameathirika kwa sababu mizigo inasafirishwa kwa kutumia SGR. Kwa hivyo, tunaomba Kamati ya Barabara na Usafirishaji ilivalie njuga hili swala na kuliangalia kwa kina ili tulimalize mara moja kwa sababu uchumi wetu unaharibika. Tumesoma kwa vyombo vya habari na kwa magazeti ya kwamba usafirishaji wa shehena kwa SGR ni ghali mno kuliko wa malori. Kwa nini wanabiashara wetu walazimishwe kutumia SGR? Tunasoma magazetini kuwa kuna wizi mwingi katika usimamizi wa SGR. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Taarifa hii. Naomba kwamba wakati Katibu Mkuu ataitwa kuja hapa, tukutane sote tumuulize haya maswali magumu."
}