GET /api/v0.1/hansard/entries/993936/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 993936,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/993936/?format=api",
    "text_counter": 30,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Kama kuna kitendo kilichofanywa na Serikali cha kuumiza husuan watu wa Pwani na uchumi wao ni miradi wa SGR. Hivi sasa, hakuna uchumi wa eneo la Pwani. Huo ndio ukweli wa mambo. Kabla ya mradi huu, Mombasa ilikuwa na biashara na nafasi ya kazi nyingi. Serikali ilianzisha mradi huu na ikawa na deni. Leo hii deni hili ni mzigo kwake. Serikali yenyewe inaona shida kuilipa. Tukiangalia hayo maagizo yaliyotolewa na Wizara ya Uchukuzi kwamba watu wasitumie malori na watumie SGR kusafirisha mizigo yao hayaungwi mkono na sheria yoyote ya Kenya. Kusema ukweli, mradi huu wa SGR umefanya watu wetu kuathirika sana. Si wenye magari ambao wameathirika pekee yao. Wenye magari wameajiri madereva ambao wana familia zinazowategemea. Baba ndiye tegemeo la familia yake kwa kuleta chakula, kulipa karo ya shule na kadhalika. Wengi wako katika vyuo vikuu na wanategemea baba yao kwa mahitaji yao ya kila siku. Namshukuru sana, ndugu yangu, Sen. Faki, kwa kuleta Taarifa hii. Ni lazima Kamati ya Barabara na Uchukuzi iweze tutatua jambo hili mara ya kwanza na mwisho. Bi. Spika wa Muda, mimi mwenyewe nilikuwa katika mkutano huo. Yule Katibu Mkuu alituhakikishia kwamba maagizo hayo yatafutwa kikamilifu. Alituambia si SGR peke yake ambao itatumika katika usafirishaji wa mizigo bali malori yatatumika. Kama viongozi wa kutoka Pwani, hasa viongozi wa siasa, ni jambo la kuhuzunisha baada ya The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}