GET /api/v0.1/hansard/entries/993937/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 993937,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/993937/?format=api",
"text_counter": 31,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "kukubiliana tukadhani jambo hili lingepata suluhisho ya kudumu. Ni unafiki kuona kwamba hakufuata makubaliano yetu. Wakati huu SGR inaendelea kubeba mizigo ikiwakandamiza watu wa Pwani. Jambo la mwisho ni upande wa uhalifu. Ikiwa mimi sina kazi, sipeleki lori, watoto wangu wamefukuzwa shule, wale mabarubaru ambao wako kwa nyumba watafanya kazi gani? Hapo ndipo chanzo cha uhalifu. Kaunti za Mombasa, Kilifi, Malindi, Kwale na Taita Taveta kuna visa vingi vya uhalifu. Hii ni kwa sababu vijana wadogo wamekosa kazi. Wazee wao wako nyumbani wakingojea chakula kutoka kwa Serikali, hususan wakati huu wa homa ya COVID-19. Serikali inajaribu kulisha watu, lakini watu wengine wanaachishwa kazi kwa sababu ya mradi huu wa SGR. Nina imani Kamati ambayo inaongozwa na ndugu yangu, Sen. Wamatangi, ni muhimu sana. Yeye ni jemedari kwa mambo haya na atafanya kazi nzuri. Tunataka ajikakamue ili aone kwamba jambo hili limefikishwa mwisho na suluhisho ya kudumu ipatikane."
}