GET /api/v0.1/hansard/entries/993961/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 993961,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/993961/?format=api",
"text_counter": 55,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa ya kuchangia taarifa ambayo imeletwa Bungeni na Seneta wa Bungoma, Sen. Wetangula. Nilikuwa na Taarifa kama hiyo ambayo nilikuwa nimewasilisha lakini nikaambiwa ya kwamba Sen. Wetangula alikuwa ametayarisha Taarifa kama hiyo. Bi Spika wa Muda, tatizo la madereva kusongamana katika mpaka wa Malaba ni tatizo ambalo limekuwa sugu sasa. Hii ni kwa sababu kwa muda wa wiki mbili, magari yamekuwa yakizuiliwa. Madereva wengi ambao ni Wakenya wanapata shida kwa sababu hawawezi kuingia Uganda bila kuwa na kibali cha kuonyesha kwamba wamefanyiwa uchunguzi wa korona, na wakapatikana kuwa hawajaambukizwa ugonjwa huo. Bi Spika Muda, hili ni tatizo la Serilkali. Hii ni kwa sababu hawajakuwa na uwezo wa kuweka vituo vingi vya uchunguzi wa korona ili madereva wetu wasiweze kupata msongamano barabarani wakati wanapoingia na kutoka. Wiki iliyopita kulikuwa na mzozo katika Kaunti ya Mombasa ambapo walikuwa wamefungua kituo cha kuchunguza madereva katikati ya makaazi ya wananchi. Wananchi walilalamika na kusema kwamba madereva, ambao huwa karibu 600 kwa siku hufanyiwa uchunguzi na mahali penyewe ni padogo hapawezi kuchukuwa hata dereva 100 kwa wakati mmoja. Kwa hivyo, baada ya kuingiliwa na Mbunge wa eneo la Jomvu, Mhe. Bady pamoja na sisi, walikubali kuhamisha kituo cha uchunguzi kutoka ndani ya Estate ya Miritini na kuweka katika Vehicle Inspection Unit ambayo iko barabarani. Hiyo haikuweza kutatua tatizo kwa sababu wale madereva wakifika katika mpaka wa Malaba, wanazuiliwa kuingia kwa sababu madaktari wa Uganda hawaamini kama ule uchunguzi ambao umefanyika Mombasa uko sawa. Mhe. Spika, hili ni swala ambalo lazima Serikali zote tatu za Jumuia ya Afrika Mashariki zinatakiwa kutatatua. Hii ni kwa sababu hatuwezi kupeleka mizigo hadi mpakani ilhali madereva wanasumbuliwa. Kuna visa ambavyo madereva ambao wameingia Uganda wamepigwa na maafisa wa usalama wa Uganda. Wengine The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}