GET /api/v0.1/hansard/entries/993962/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 993962,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/993962/?format=api",
    "text_counter": 56,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "wamepokonywa mali. Wengine wanalala na kupika barabarani, ambapo ni hatari kwa bidhaa za mafuta kama vile petroli na gesi ambazo zinasafirishwa na magari yale. Hili limekuwa swala sugu na ni lazima tutafute ufunguzi wa haraka kwa sababu ni madereva wetu ndio wanapata shida. Vile vile, ikiwa halitatatuliwa kwa haraka, ugonjwa wa korona utajaa katika barabara zote za Mombasa na Malaba. Kwa sababu Serikali haijakuwa tayari kuweka vifaa vya kutosha ili madereva waweze kuchunguzwa na kupeana vibali vya kusafiri, cheti cha Yellow Fever kinahitajika ukiingia Uganda. Kwa nini hawasemi hawakubali cheti hicho kwa sababu imetoka Kenya? Wanakataa vyeti vya Kenya za COVID-19, lakini wanakubali vyeti vya Yellow Fever. Kwa hivyo, kama vyeti vya Yellow Fever vinakubaliwa, vile vile vyeti vya COVID-19 vya Kenya lazima vikubaliwe ili biashara isiharibike kati ya Kenya na Uganda. Asante kwa kunipa fursa hii."
}