GET /api/v0.1/hansard/entries/993964/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 993964,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/993964/?format=api",
"text_counter": 58,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13200,
"legal_name": "Issa Juma Boy",
"slug": "issa-juma-boy"
},
"content": "Asante Bi Spika wa Muda. Nasimama pia kuunga mkono Taarifa hii ambayo imesomwa na Sen. Wetangula. Shida hiyo pia imepata watu wa Kaunti ya Kwale. Mpaka wa Kenya na Tanzania kule Kaunti ya Kwale uko Lunga Lunga na Horo Horo. Ukifika Horo Horo, malori na magari mengine yameanzia Horo Horo hadi Lunga Lunga kule juu, karibu na Isolation Centre. Ukiangalia, hili si jambo ambalo haliwezi kutatulika, bali ni lazima sisi kama Maseneta na viongozi wengine, tuweze kupiga kelele ili Serikali iweze kutatua mzozo huo. Kama Sen. Wetangula na Sen. Faki walivyosema, hii shida ni lazima sisi kama viongozi tusimame kidete kwa sababu hatuwezi kukaa tukiona malori yameezekwa pale kwa muda wa zaidi ya wiki moja, ilhali kuna COVID-19. Katika Kaunti ya Kwale, kuna kesi mbili za COVID-19 ambazo zimetokea karibu na hao madereva wa malori. Mimi naunga mkono Taarifa hii na Kamati inayoongozwa na Sen. Wamatangi iweze kushughulikia ili jambo. Tunataka Waziri aje hapa tumhoji na tumueleze, ili shida hii itatulike kwa haraka. Asante."
}