GET /api/v0.1/hansard/entries/994116/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 994116,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/994116/?format=api",
"text_counter": 210,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuunga mkono ripoti ya sita ya Kamati maalum ya COVID-19. Kwanza, ningependa kumpongeza Mwenyekiti wa Kamati hii. Tumeweza kufanya mikutano zaidi ya 55 kwa muda mchache. Katika mikutano hiyo yote walihudhuria ilikuwa wazidi asilimia 70 katika kila mkutano. Kwa hivyo, imeonyesha ya kwamba Maseneta ambao wako katika kamati hii pamoja na wafanyikazi wa Bunge ambao wanatumikia Kamati hii wamejitolea asilimia mia kwa mia katika kuihudumia. Mbali na kupongeza Mwenyekiti na Maseneta wote ambao wako katika Kamati, pia nawapongeza wafanyikazi wa Bunge ambao wako seconded katika Kamati ile. Kamati imeweza kufanya mahojiano na washika dau tofauti. Isipokuwa Waziri wa Elimu ndiye pekee amekataa kuhudhuria vikao vya Kamati yetu. Ijapokuwa Mwenyeketi aseme ni rafiki yake, itakapofika wakati wa kuweka kiboko nafikiri atamweka kiboko Waziri (Prof.) Magoha kwa kupuuza wito wa Bunge. Ni haki ya wananchi ya kuangalia shughuli za Serikali katika mambo wanaofanyia wananchi. Bi. Spika wa muda, unyanyapaa yaani stigma ndio tatizo kubwa ambalo linatuathiri katika vita dhidi ya COVID-19. Wengi wana hofu kwamba ukiambiwa umepatikana na korona ni kama ambaye umepewa hukumu ya kifo na hustahili kufanyiwa jambo lolote na Serikali. Ningependa kusema kwamba korona ni ugonjwa kama magonjwa mengine. Unapoambukizwa corona una asilimia tisaini na nane kwa mia kwamba unaeza kupona kwa hivyo ni asilimia mbili pekee ndio inatutia hofu kwamba hatutaweza kuishi maisha ya kawaida. Wengi wanaopatikana na virusi vya corona inabidi jamii iwatenge. Jamii inapowatenga ina maana kwamba hawataweza kuwa na nafasi ya kuweza kupata fursa ya kujihudumia kwa ugonjwa ule na jamii pia iweze kuwasaidia katika kujitibu ama kupona. Lazima tupambane na unyanyapaa ili tuweze kuuza sera kwamba ugonjwa wa korona ni ugonjwa kama ugonjwa mwingine wowote. Tukiangalia hapo mbeleni tulikuwa na ugonjwa wa UKIMWI ambao ukipatikana na UKIMWI na ufe, unazikwa kwa manyloni mpaka ikapatikana kwamba shida kubwa tuko nayo katika UKIMWI ni unyanyapaa. Tulipopambana na unyanyapaa tukaleta vifaa zile centre zinatoa huduma za"
}