GET /api/v0.1/hansard/entries/994122/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 994122,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/994122/?format=api",
    "text_counter": 216,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "wanakwenda karantini na wale wanalazwa hospitali kutibiwa ugonjwa wa korona. Kwa hivyo, wengi waliogopa kuchukua hatua ya kufanya uchunguzi na ndio maana ikawa uchunguzi unafeli. Swala la kufanya cessation of movement yaani kuzuia watu wasiingie na kutoka old Town na Eastleigh, sheria hii ilichukuliwa bila kufanya mashauriano na wakazi wa sehemu zile. Sehemu yoyote kama vile Sen. Sakaja alitangulia kusema ikifanywa uchunguzi sasa itapatikana kwamba asilimia mbili na nusu ama asilimia tatu ya wananchi katika eneo lile wana virusi vya korona. Kwa hivyo, ni virusi watu wanaishi navyo lakini havijaambukiza ikafika kiwango ambacho watu wanapata ugonjwa wa korona na kuweza kuathirika na kulazwa hospitali na watu kufariki. Ilikuwa ni makosa kwa Serikali kulazimisha cessation of movement katika old town na Eastleigh. Hii ni kwa sababu imeathiri watu wengi katika huu mwezi wa Ramadhan. Wengi wao walitarajia watapata biashara siku za mwisho za Ramadhan ili waweze kujikimu kimaisha na waangalie jamii zao kwa muda wa miezi mitatu au minne itakayofuatia mbeleni. Watu wa biashara wote wamepoteza biashara zao. Wakati huu, Serikali haijatoa mpango wowote wa kuhakikisha kwamba wamepata ridhaa kwa kukosa biashara. Katika Ripoti hii, tumezungumzia swala la madereva wanaopeleka bidhaa katika nchi za nje na wale wanaoleta bidhaa katika nchi ya Kenya. Madereva wetu wengi wamekwama katika sehemu za Namanga, Malaba na Lunga Lunga kwa sababu nchi jirani zimekataa kuwaruhusu kuingia mpaka wachunguzwe katika nchi zile ile waweze kupata vibali vya kuingia. Kama tungekuwa tumefanya mipango ya mapema, tungeweza kuweka vifaa hivi vya uchunguzi katika kila weighbridge. Magari yote yakitoka Mombasa kwa mfano kuna weighbridge Mariakani, Dongo Kundu, Mlolongo na kwingineko. Weighbridges zingekuwa zinatumika watu kuchunguzwa na ukipewa kibali kile kiweze kutumika kwa muda wa mwezi mmoja ili mtu asiweze kuwa ana haja ya kuchunguzwa tena baada ya siku 14. Hii imekuwa shida kuhakikisha ya kwamba watu wale wanapata huduma ya kuchunguzwa kwa haraka na kwa njia ambayo haitasababisha maambukizi. Jomvu Constituency ilikuwa ni kituo kimoja ambacho kina wahudumu wawili pekee na kinahudumia watu zaidi ya 600 kwa wakati mmoja ili kuhakikisha kwamba watu wamepimwa kwa haraka wawezwe kupata matibabu. Kutokana na msongamano ulioko Malaba na hatua nyingine ambazo Waziri amechukua kwa kisingizio cha korona, maandamano ya black Monday katika Mji wa Mombasa yatarudi tena kuanzia Jumatatu tarehe moja mwezi wa sita. Hii ni kwa sababu Serikali imeshindwa kutatua tatizo la madereva wa long distance driving kupeleka mizigo nchi za nje. Pia wameshindwa kutoa nafasi kwa biashara iweze kufanyika bila ya mapendeleo ya Standard Gauge Railway (SGR). Katika kuingiliana na washika dau tofauti, Serikali haikuwa na mwelekeo mwanzoni kuhusiana na swala la virusi vya korona. Mwanzoni walisema kuwa kila mtu atalipishwa ili afanyiwe test ya korona. Watu walipopiga kelele wakageuka wakasema kwamba sasa test zitakuwa bure. Walisema watalipisha watu wanaokwenda katika karantini. Baadaye, wananchi walipolalamika wakasema ya kwamba sasa itakuwa bure. Kumekuwa na kutoelewana kwa upande wa Serikali kuhakikisha kwamba wananchi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}