GET /api/v0.1/hansard/entries/994126/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 994126,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/994126/?format=api",
    "text_counter": 220,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Swala la kijana ambalo Sen. Sakaja alizungumzia ni kitu ambacho kiko wazi katika macho ya wananchi, kwamba polisi walitumia silaha kinyume na sheria kwa sababu walipiga risasi wakati ambao haukuwa salama. Wananchi wanaendelea kupata shida katika sehemu nyingi. Kwa mfano, tumeona ripoti leo kwamba katika sehemu za Old Town na Eastleigh watu wanawalipa askari polisi ili waweze kuingia na kutoka kwa sababu ya maswala ya Virusi vya Korona. Mhe. Bi. Spika wa Muda, vile vile, tumeona kwamba biashara katika zile kaunti ambazo hazikuwekwa cessation of movement imepungua pakubwa. Nimesafiri leo asubuhi kutoka Mombasa kuja Nairobi. Nimeona kwamba sehemu za Ukambani, kuanzia maeneo ya Mtito Andei mpaka Mlolongo, kuna chakula kingi sana, ikiwemo matunda na vyakula vingine vingi lakini hatuoni wafanyabiashara wakichukuwa fursa hiyo kuleta bidhaa zile. Mfano ni Kaunti ya Taita-Taveta na zinginezo ambazo hazina cessation ofmovement ya biashara. Pia, tumeona kuwa Serikali imezembea katika maswala ya afya kwa sababu huduma zilizokuwa zikitolewa katika zile sehemu za Karantini zilikuwa haziridhishi kabisha. Tukiangalia kama kule Port Reitz kulikuwa na karantini ya Serikali ambayo ilikuwa haina huduma za maji. Kaunti nyingi zimeamka sasa na kutoa huduma ya maji kwa wananchi. Kabla ya kuja kwa Virusi vya Korona huduma ya maji ilikuwa ni nadra sana katika sehemu zingine za kaunti zetu. Tukiangalia Mombasa, soko la zamani la Marikiti ambalo lilijengwa katika miaka ya 1900 limepewa sura mpya sasa kwa sababu ya Virusi vya Korona. Kabla ya hapo kulikuwa na utepetevu mkubwa sana katika utendakazi wa Kaunti ya Mombasa na vile vile vitengo vya Serikali ya Kenya katika Jiji la Mombasa. Hakukuwa na huduma kubwa, kwa mfano, kulikuwa na ukosefu wa maji, barabara mbovu na huduma za usafi katika soko kutepetea. Ijapokuwa Korona ni janga, limeweza pia kuleta Silver lining katika baadhi ya kaunti zetu ili kuona kwamba huduma zinaboreshwa. Hapa kumezungumziwa swala la watu walioko nje ya Kenya. Ni kweli Wakenya wengi walioko nje ya nchi wametatizika kwa sababu hakuna ndege za kuwarejesha Kenya. Nchi zingine kama vile Uingereza na Marekani zimetuma ndege kubeba raia wao waliokuwa katika sehemu tofauti tofauti ambako walikuwa wamekwama kwa sababu ya janga la Korona. Wale marubani wanne The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}