GET /api/v0.1/hansard/entries/994127/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 994127,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/994127/?format=api",
    "text_counter": 221,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "ambao walikuwa katika ile ndege iliyoshambuliwa na jeshi la Ethiopia walikaa Mogadishu kwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu bila kazi. Hiyo ndiyo ilisababisha kutoweza kurudi nyumbani kujiunga na familia zao. Kazi ile ilipotokea, ilikuwa mara yao ya kwanza mwezi ule na wakashambuliwa na kufariki. Tumeona kwamba swala la Wakenya kurejea nyumbani wakati huu ambao kuna shida limetatiza Serikali. Ijapokuwa Serikali inategemea zile foreign remittance s ili kuinua hali yake ya fedha za kigeni, sasa imewatupa mkono watu wengi ambao wako nje kwa sababu hawakuweza kuwarejesha nyumbani kujiunga na familia zao. Ripoti yetu ya Sita ambayo imetolewa imechangiwa pakubwa na washika dau wengi. Vile vile katika upande wa Mahakama kumekuwa na ongezeko la matumizi ya teknolojia kwa sasa. Leo nilipokuwa nikisafiri kutoka Mombasa kuja Nairobi nilichukuwa judgement kwa kesi yangu moja ambayo ilikuwa inasomwa kutoka Mombasa kupitia kwa mtandao. Hiyo imewezesha kesi nyingi kuamuliwa kupitia kwa mitandao kwa sababu ni rahisi na haina gharama. Haimlazimishi hakimu kujitokeza hadharani na kujiweka katika hatari ya kuambukizwa Virusi vya Korona. Ipo haja katika siku za usoni kuhakikisha kwamba teknolojia kama hii inaendelea kutumika mahakami. Ukiangalia katika ratiba ya kesi ambayo inaorodheshwa kila asubuhi, utapata kuwa kuna kesi zaidi ya 20 ama 30 ambazo zinatajwa ili kutoa mwongozo wa jambo linalotakikana kufanyika. Kesi zile hazina haja kumpeleka wakili mahakamani ama hakimu aje katika mahakama ya wazi, ili kufanya maswala kama yale. Zinaweza kufanywa kupitia kwa mtandao mara moja kati ya Saa Mbili na Saa Tatu, ili Saa Tatu mahakama ianze kazi ya kusikiliza kesi kwa haraka na wananchi wapate huduma za mahakama kwa urahisi. Swala lingine ambalo limezungumziwa ni social programmes kwa wazee na wale wengine ambao wameathirika. Ni kweli kuwa hata katika orodha ya mawakili katika nchi ya Kenya kuna wengi ambao hivi sasa wametatizika kwa sababu hawajaweza kupata kazi inayowawezesha kupata malipo kutokana na huduma zao. Nimefurahi kwamba baadhi ya mawakili katika Law Society of Kenya (LSK) wamefanya michango na kuwasaidia wale ambao mapato yao yamekuwa chini, ili waweze kujimudu kimaisha kwa muda huu wa janga la Korona. Hayo hayatoshi. Ipo haja ya kuangalia ni njia gani ambazo tunaweza kuanzisha hazina maalumu ya kusaidia biashara ndogo ndogo kama za wale"
}