GET /api/v0.1/hansard/entries/994206/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 994206,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/994206/?format=api",
"text_counter": 37,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "huwa ni kama baraka kutoka kwa Mungu. Wanajua vile wanavyoyatega na vile yanawapatia mazao. Lakini ukija Kenya, nchi iliyobarikiwa na Mwenyezi Mungu na mchanga wake ni ule ambao watu wanaweza kupanda na kuzoa mazao ambayo yatawaangalia katika maisha yao ya usoni. Mtihani huo Serikali yetu imeanguka. Bw. Spika wa Muda, yale mafuriko yanaweza kutengenezwa kwa njia ambayo tuko na mabwawa ambayo yanaweza kuyatega yale mafuriko, lakini tunawacha kutega haya maji na yanakuwa gharika. Gharika inafanya mito kufurika, kuharibu mimea na kupoteza maisha ya binadamu. Haya ni mambo ambayo tunaona na ni aibu. Kila mwaka tunajua kwamba, itakapofika mwezi wa pili, tatu, na nne ni lazima Wakenya watakufa kwa sababu ya mito kufurika na maji kuwa mengi na mazao yatapotea. Wakulima katika upande wa Kitale na kila mahali katika Kenya yetu wameathirika ajabu. Zaidi sana nikiongea habari ya Lamu, ni kwa wale ambao wana shida. Hivi sasa kule Lamu ni kama ambako kumesahauliwa kana kwamba, si Kenya tena. Hi ndio sababu watu wa Lamu wanateseka. Wengi wamewahi kupoteza maisha yao. Ninasema hivyo kwa uchungu kwa sababu katika Katiba ya Kenya, ikiwa wewe ni Mkenya, ni jukumu la Serikali kuangalia uhai wako. Tunaona makosa kama haya kule Lamu, Kilifi, upande wa Magharibi na sehemu mbali mbali. Watu wameathirika sana. Ni jambo la aibu katika ulimwengu mzima kuona kwamba Wakenya wanapoteza maisha yao kwa sababu ya mafuriko."
}