GET /api/v0.1/hansard/entries/994220/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 994220,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/994220/?format=api",
    "text_counter": 51,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Malalah",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13195,
        "legal_name": "Cleophas Wakhungu Malalah",
        "slug": "cleophas-wakhungu-malalah-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika wa Muda. Kwanza ninampongeza ndugu yangu Sen. Loitiptip kwa kuleta Hoja hii. Mambo ya mafuriko katika nchi yetu ni shida ambayo imekuwa ikitokea kila uchao. Hii sio mara ya kwanza Kenya kuwa na mafuriko. Tangu niwe mtoto mdogo hadi sasa hivi, kila mwaka tunalia kwa sababu ya mafuriko ambayo yanaangamiza watu wetu. Ni lazima sisi viongozi tuwajibike na tuwe na mikakati ya kuhakikisha tumekomesha maswala haya ya mafuriko ambayo yanakuja kila mwaka. Bw. Spika wa Muda, kwa mfano, eneo la Magharibi, hakuna bwawa hata moja katika Mto Nzoia, ilhali kila mwaka tunalia kwamba, Budalangi, Matungu, Mumias West na Likuyani kuna mafuriko. Mimi kama Seneta wa Kaunti ya Kakamega ninapendekeza wakati tunatengeneza Bajeti ya kitaifa ni lazima tuangazie maswala ambayo yatasaidia mwananchi wetu. Itakuwa makosa kwamba Bajeti ya mwaka 2020/2021 ikose bwawa katika Mto Nzoia. Tunajua vizuri Serikali inafaa iwajibike kulinda wakaazi wa Mkoa wa Magharibi. Kwa hivyo, ninahimiza kwamba watu ambao wako katika nyadhfa za kuhakikisha wamepeana raslimali za kutosha, watenge pesa za kutosha kuweka bwawa katika Mto Nzoia ili mwaka ujao, mafuriko yasiangamize watu wetu. Viongozi katika bunge za kaunti wanapotengeneza makisio ya bajeti ya 2020/2021, ni lazima waangazie mikakati ya kuchochea uchumi wetu. Kwa lugha ya kimombo tunaita economic stimulus projects. Zile bajeti wanazozileta katika bunge za kaunti zinafaa kuangazia maswala ambayo yatasaidia mwananchi wa kawaida baada ya janga la mafuriko na Coronavirus . Bw. Spika wa Muda, tuko na uhakika ya kwamba, mafuriko haya na janga la"
}