GET /api/v0.1/hansard/entries/994222/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 994222,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/994222/?format=api",
    "text_counter": 53,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Malalah",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13195,
        "legal_name": "Cleophas Wakhungu Malalah",
        "slug": "cleophas-wakhungu-malalah-2"
    },
    "content": "yamefanya vijana wetu kupoteza ajira na wamama kupoteza biashara zao. Kwa hivyo, ni jukumu letu kama viongozi wa Bunge la kitaifa na bunge za kaunti, kuhakikisha kwamba makisio ya bajeti 2020/2021 yameangazia mambo ya kuimarisha uchumi wa Kenya. Kwa mfano, makisio ya bajeti ya 2020/2021 katika Kaunti ya Kakamega hayajaangazia kikamilifu mapendekezo ya kusaidia watu ambao nyumba zao zimebomoka. Wametenga Kshs3 milioni kuangazia familia ambazo zilitoka katika boma zao. Ningependa bunge za kaunti ziweke pesa za kutosha ili wasaidie wananchi ambao wanahitaji pesa za kujenga. Shilingi milioni tatu hazitoshi. Ningependa waakilishi wa bunge za kaunti na wale wanaohitajika kuweka pesa katika sekta ya kusaidia familia ambazo zimeathirika waweke pesa za kutosha. Serikali za kaunti zinafaa kubuni njia ya kuhakikisha vijana wamepata kazi. Tunashukuru Wizara ya Devolution ikiongozwa na Cabinet Secretary, Wamalwa kwa kuleta chakula cha kutosha Kakamega na maeneo mengine, lakini chakula pekee hakitoshi. Watu wanahitaji matibabu ya kutosha na fedha katika mifuko zao. Serikali Kuu ilitoa pesa kwa wale wasiojiweza. Lakini, ningependa walioadhirika na mafuriko wakuwe katika mstari wa mbele kupokea pesa hizo. Wale ambao wako The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}