GET /api/v0.1/hansard/entries/994223/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 994223,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/994223/?format=api",
    "text_counter": 54,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Malalah",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13195,
        "legal_name": "Cleophas Wakhungu Malalah",
        "slug": "cleophas-wakhungu-malalah-2"
    },
    "content": "Shibale Primary School, Mumias, ndio wanafaa kuwa katika mstari wa mbele kupokea pesa kutoka kwa Serikali. Wale ambao wanaishi kwa nyumba zao wasipate pesa, ilhali wanaoishi kwa mashule na makanisa kwa sababu ya mafuriko wanakosa pesa. Ninaomba Serikali iangazie watu ambao wanaishi Likuyani Primary School ili wapate pesa kwanza ndio tuanze kugawia watu wengine ambao wanaishi katika nyumba zao. Ninapongeza ndugu yangu Seneta wa Kaunti ya Lamu. Watu wa Lamu wako na kiongozi ambaye anawasikia na kuwawakilisha. Ningependa aendelee kufanya kazi yake vyema na kuwakilisha watu wake ambao wameadhirika kwa sababu yewe alichaguliwa kufanya kazi hiyo. Ninampongeza pia Seneta wa Kisumu ambaye amezoea kutetea watu wake. Kipengele 96 Cha Katiba yetu kinasema kwamba ni jukumu letu kuwakilisha wananchi wetu katika Bunge hili. Mimi kama Seneta wa Kaunti ya Kakamega nimesimama leo hapa kuwakilisha watu wangu. Ni lazima Serikali itume pesa kuhakikisha ya kwamba familia hizo ambazo zimeathirika katika kaunti yangu na Mkoa wa Magharibi kwa jumla wamefaidika."
}