GET /api/v0.1/hansard/entries/99435/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 99435,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/99435/?format=api",
    "text_counter": 260,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ms. Leshomo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Kwanza, ningependa kumshukuru sana mhe. Lekuton kwa kuleta Mswada huu hapa Bungeni. Sisi sote tunaunga mkono Mswada huu. Huu ni Mswada ambao utawasaidia sana wafugaji wa mifugo. Ni jambo la kuhuzunisha mno kuwa tangu Uhuru hatujawahi kama nchi kuwa na sheria kama hii inayopendekezwa na Mswada huu. Ninaomba kila mhe. Mbunge katika Bunge hili kuunga mkono kikamilifu Mswada huu kwa sababu wafugaji wamekuwa na shida nyingi tangu Uhuru. Wizi wa mifugo umeleta madhara makubwa kwa wafugaji na wanyama wao. Wanyama wetu huhaangaishwa sana na wezi wa mifugo. Wanaibwa kutoka wilaya moja hadi nyingine. Hakuna sheria inayolinda wanyama wetu. Wanyama wetu wanapoibwa, huenda masafa marefu bila maji na chakula. Kupitia Mswada huu tutapata maofisa watakaotibu na kulinda wanyama wetu. Sisi sote tunajua nyama na maziwa ni muhimu sana katika afya ya mwanadamu. Kwa hivyo, tungependa wanyama wetu watunzwe vizuri na maofisa hawa. Tukifanya hivo, watu wetu watakuwa na afya nzuri. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa sababu ya ukosefu wa maofisa hawa wa mifugo, wafugaji wamekuwa “madaktari” wenyewe kwa sababu ya taabu. Mara nyingi utamuona mfugaji akinunua dawa lakini hana ujuzi wowote wa kutibu ng’ombe. Hii ni hatari sana kwa yeye mwenyewe na ng’ombe huyo. Wakati mwingine, ng’ombe anapofariki akitibiwa, mfugaji huchinja ng’ombe. Yeye na familia yake na majirani hula ng’ombe huyu. Hii ni hatari sana. Watu wengi wamekufa kwa kula ng’ombe waliokufa wakitibiwa na wafugaji. Ni sheri kama hii ambayo tunataka kupitisha hapa ambayo itawawezesha watu wetu kuwa na madaktari wa afya ya wanyama waliyohitimu karibu nao. Kwa hivyo, tunahitaji wafugaji au watu wetu wapate masomo kuhusu ufugaji wa wanyama kwa sababu madatari kutoka mijini hawapendi kuishi nasi kwa sababu ya ukavu wa sehemu zetu. Pia wafugaji huuza ngozi za wanyama wao kwa Kshs30. Lakini ngozi hii ikisafirishwa nje ya nchi, inauzwa kwa zaidi ya Kshs30,000. Ninaamini sheria hii itawasaidia watu wetu kupata soko ya ngozi za wanyama wao. Ni ombi langu tuwe na viwanda vya nyama karibu nasi ili tuuze nyama, maziwa na ngozi kwa bei nafuu. Serikali itusaidie kuona ya kwamba mifugo wetu wanasafirishwa moja kwa moja hadi Kenya Meat Commission (KMC). Hii ni njia mojawapo ya kuwasaidia wafugaji wa wanyama. Bw. Naibu Spika wa Mda, kwa kweli, watu walioumia zaidi ni wafugaji. Hawana maji ama chochote karibu kwa matumizi ya ng’ombe na mbuzi wao."
}