GET /api/v0.1/hansard/entries/994640/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 994640,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/994640/?format=api",
"text_counter": 276,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": " Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa tu wenzangu waniazime masikio yao. Kwanza, nataka kuchukua fursa hii kushukuru dadangu Mhe. Sabina na Kamati ya Afya. Nikiangalia Hoja kwa undani, hii kamati maalum imepatiwa nyadhifa gani inazidi mipaka ya ile ya afya? Ndani yake kuna masuala ya uchumi. Ndani yake kuna masuala yenye kuhusika na kitu gani kitaweza kufanywa baada ya hili janga la corona kumalizika? Kwa hivyo, mimi kibinafsi, na nina imani wengi hapa watakubaliana nami, napendekeza kuwa tuikubali Hoja hii kwa kauli moja sote na kwa minajili ya Kenya. Nimeona dadangu kutoka Mombasa, Mbunge wa Likoni, ni moja wa wale ambao watakuwa katika kamati hii maalum. Ningeomba wasistize mambo sita zaidi. Kwanza, uchumi wa watu wetu. Pili, ni lazima tushinikize ya kuwa nchi ifunguliwe sasa hivi. Hali ya uchumi vile ilivyo, hali ya watu na nafsi zao na bugdha walizonazo, zinaleta changamoto mno. Ni lazima nchi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}