GET /api/v0.1/hansard/entries/994641/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 994641,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/994641/?format=api",
    "text_counter": 277,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mvita, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": "ifunguliwe. Katika kufunguliwa, ni lazima Kamati ya Afya iweze kuangalia masuala haya. Waweze kukubaliana na kupitisha Miswada ambayo itakubalika ya kuwa ikiwa nchi itafunguka, basi wale wa kufanya kazi na wananchi kwa ujumla, ikiwemo sisi Wajumbe, iwe ni sharti tuhakikishe hali zetu za afya ziko sawa. Ikiwa hatujijali, sisi tujali hali ya wale wengine. Ikiwa tunasema yule mwenye M-Pesa aweze kupimwa, na sisi pia tunahusiana na watu ambao wako mashinani, tujue hali zetu kwa sababu ya watu wetu. Ni raha tena sana kwa sababu katika maeneo yaliyofungwa, licha ya kuwa katika hali ya mchipuko mchipuko wa hapa na pale wa kuzungumza na bugdha, pengine ikaweza kuchukuliwa ya kuwa Abdullswamad Sherrif Nassir ama Gavana wa Mombasa wana nguvu za kisheria kufunga mji. Nataka hii kamati iweze kuweka kinagaubaga. Na iweke kinagaubaga, sehemu ya Old Town na Eastleigh zilipofungwa, natija yake ilikuwa ni nini? Lengo lilikuwa ni lipi? Je, tuliweza kuhakikisha ya kuwa tumelifikia lile lengo letu? Hivi tunavyozungumza, kuna sehemu zingine za Kenya hii, na tunawaombea Mwenyezi Mungu… Hatujalii mtu yeyote mabaya. Lakini kuna baadhi ya sehemu nyingine katika Kenya hii watu zaidi wamepata mchipuko wa maradhi haya, lakini hatusikii kuwa sehemu zile zimefungwa. Kwa hivyo, ni lazima hii kamati iweze kutuambia kinagaubaga lengo la kufunga Old Town na Eastleigh lilikuwa ni nini. Kama madhumuni yalikuwa ni kufika sehemu hii, tulifika ama hatukufika? Na ikiwa tulifika tuambiwe hesabu vile ilivyo. Na ikiwa hatukufika pale, basi ni kwa nini kuongezwa ule muda wa kufungwa? Ni lazima kuangaliwe njia muafaka—kwa lugha ya Kiingereza tutasema protocols . Sehemu zetu za ibada zikifunguliwa, watu watarejea vipi katika sehemu zile? Kamati hii ifanye kazi pamoja na makasisi, maimamu, na pundit wetu, ambao kwa lugha nyingine ni wale wa kuongoza katika temples ama baniani. Nikimalizia, ni ombi langu kuwa, tukiwa tunafungua mashule, vyuo na taasisi, lazima tuhakikishe kuwa athari hii isiongezeke zaidi. Kwa hayo yangu, nawasihi, nawaomba na nawanyenyekea tusiwekwe katika matakwa ya kamati moja na nyingine ikawa ni yenye kuziba matakwa ya Wakenya wote. Ni ombi ambalo nina imani ni la wengi walioko. Tena tunasistiza ya kuwa katika siku ambazo kuna bugdha, mtu yeyote ambaye kidogo anaona ana akili ataweza kuleta bugdha za kisiasa na jasho la kisiasa. Lakini hekima ni kuweza kuleta utuluvi katika sehemu ambayo iko na bugdha tayari. Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}