GET /api/v0.1/hansard/entries/994666/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 994666,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/994666/?format=api",
"text_counter": 302,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ganze, ODM",
"speaker_title": "Hon. Teddy Mwambire",
"speaker": {
"id": 13334,
"legal_name": "Teddy Ngumbao Mwambire",
"slug": "teddy-ngumbao-mwambire-2"
},
"content": " Ahsante sana. Ningependa kufahamisha Waheshimiwa kwamba Hoja hii hailengi kudhalilisha ama kuharibia kazi ya kamati yoyote, lakini inasaidia kuweza kupambanua ujuaji na hali sawa ambayo itaweza kuleta mwelekeo utakaokuwa mwema. Ningependa watu waelewe kwamba madhumuni ya Kamati hii ni kuhakikisha kwamba kila kitu kitakuwa kinafanywa kwa makini na kitu ambacho kimefuatilia utaratibu wa sheria za Bunge na sheria ambazo ziko hata kwa Katiba. Kwa hivyo, hakuna mahali ambapo pana bana mtu yeyote. Kwa hivyo, natoa ile hofu ambayo imetokea kwa baadhi ya Waheshimiwa ambao wanasema kwamba masuala kama haya yatakuwa yanabana kamati nyingine. Ningependa tuunge mkono na tuweze kufuatilia ili tuhakikishe kwamba kila pembe ya nchi na kila kitu kinafuatiliwa kikamilifu ili kusiwe na upungufu wa kuweza kupata hakikisho la wazi kwa Bunge letu la Kitaifa hususan kwa kazi ambazo inastahili kuzifanya. Ahsante, na ninaunga mkono."
}