GET /api/v0.1/hansard/entries/995020/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 995020,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/995020/?format=api",
    "text_counter": 329,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili kuchangia Taarifa ambayo imeletwa na Seneta wa Nandi, Sen. Cherargei. Swala la mauaji ya kiholela na polisi limeongezeka pakubwa katika nchi yetu. Ningependa kutoa rambirambi zangu kwa wale wote waliyofariki mpakani wa Kaunti za Nandi na Kakamega. Tarehe 30 Mei, 2020, kule kwetu pwani tulipata kisa ambapo polisi waliwaua watu wanne akiwemo mwenye nyumba hiyo, Ramadhan Mohammed Chizwa na wanawe watatu baada ya polisi kuvamia nyumba yao usiku na kuwapiga guruneti na pia kuwapiga risasi wanawe wawili, akiwemo kijana wa miaka sita, Ramadani Chiswa and msichana wa miaka minne kwa jina Raha Machiswa. Bi. Spika wa Muda, ni jambo la kusikitisha kwamba hawa waliuliwa na polisi wakiwa nyumbani kwao wakati polisi waliwavamia kama wamelala. Je, ni sababu gani polisi waliwavamia usiku bila kujua walioko ndani ni kina nani? Mtoto ambaye alikuwa kwa tumbo la mamake aliuwawa. Huu ni unyama mkubwa kuwa polisi wetu ndio wanaua wana familia na wananchi wa Kenya. Imekuwa pia ni tatizo kwa sababu hata ofisi ya Director of Public Prosecutions (DPP) haiwezi kufanya uchunguzi . Zamani, ilikuwa mtu akifa kwa njia ambayo si halali, ama si njia ya kawaida, Serikali kupitia kwa polisi walikuwa wanafanya uchunguzi ambapo hakimu anaangalia ushahidi wa vile alivyokuwa mpaka vile mtu akapoteza maisha yake. Wakati huu, hatujaona uchunguzi wowote. Katika kupambana na kafyu, zaidi ya watu 20 wameuwawa katika mikono ya polisi na hadi sasa hakuna uchunguzi wowote umefanywa ili kushtaki wale wanaohusika na mauaji hayo. Swala la watu kuuliwa kiholela katika nchi yetu si nzuri. Kule Amerika tunashuhudia maandamano. Tunaona kama haya ni mambo ya ugenini lakini hapa kwetu yanafanyika ijapokuwa sisi hatujakuwa wajasiri kiasi ili kuweza kuandamana na kupinga tendo hili la maafa ya watu wetu mikononi mwa polisi wetu. Ningeomba Kamati ya Usalama na Masuala ya Nje, iweze kushughulikia swala hili na lile la Kaunti ya Kwale. Hii ni kwa sababu tumeona maonevu mengi yanafanyika katika mikono mwa polisi."
}