GET /api/v0.1/hansard/entries/995046/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 995046,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/995046/?format=api",
"text_counter": 355,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13200,
"legal_name": "Issa Juma Boy",
"slug": "issa-juma-boy"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili nichangie Taarifa hii ambayo imeletwa na Sen. Cherargei wa Kaunti ya Nandi. Kusema kweli, hivi sasa tunavyoona nchi inavyoenda na jinsi polisi wanavyofanya si sawa. Vitendo kama hivi vinavyoendelea sasa ni kama unyama. Kama Seneta wa Kaunti ya Kwale, juzi katika sehemu ya Diani inayoitwa Kibundani, polisi walimuua bwana mmoja, mke wake aliyekuwa mja mzito na watoto wao watatu. Kilikuwa kitendo kibaya sana. Hata viongozi wengine walijitokeza na kulaani kitendo hicho. Hili jambo linatakiwa kuingiliwa kati na litazamwe kwa undani. Kwa hivyo, hii Taarifa imeletwa wakati mzuri sana. Juzi katika runinga mliona jinsi bwana yule alipigwa risasi katika sehemu ya Kibundani, Kaunti ya Kwale. Watoto wake wadogo, mke wake mja mzito na kiumbe ndani yake waliuawa pia. Tunalaani kitendo hicho. Iwapo kulikuwa na usawa, hawa polisi wangetafuta njia mwafaka na ijulikane huyo mtu angepatikana namna gani, si kutumia nguvu zaidi kama hiyo. Kamati ambayo itashughulikia hili jambo inafaa kutembelea Kaunti za Trans Nzoia, Kwale, Isiolo na kwingineko ambako hayo maafa yametokea ili watatue swala hilo."
}