GET /api/v0.1/hansard/entries/995296/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 995296,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/995296/?format=api",
"text_counter": 87,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika. Kupitia Kanuni ya Bunge 44(2)(c), naomba taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Leba na Jamii. Sote tunakubali na tunaifurahia na kuikaribisha mipangilio ya Serikali kuajiri vijana hususan wakati huu mgumu wa Corona. Katika miezi ya Aprili na Mei, vijana takriban 3,500 kutoka Eneo Bunge la Mvita waliajiriwa kupitia mpango almaarufu Hifadhi Mazingira Kazi Mtaani. Kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Leba na Jamii, kwanza Waziri mhusika atueleze kwa nini baadhi ya vijana hawa hawajalipwa. Pili, Wizara imeweka mikakati gani vijana wetu wasichelewe kulipwa na kuteswa ili kufuata haki yao. Tatu, kama Waziri anafahamu kama vijana hao wanafanya kazi bila vifaa na bila mavazi yenye kuwahifadhi. Ahsante sana, Mhe. Spika. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}