GET /api/v0.1/hansard/entries/998555/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 998555,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/998555/?format=api",
"text_counter": 1505,
"type": "speech",
"speaker_name": "Wundanyi, WDM-K",
"speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
"speaker": {
"id": 13509,
"legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
"slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Spika kwa kunipa nafasi hii. Naanza kwa kuunga mkono Hoja hii. Kama mmoja wa wanakamati wa Kamati ya Bajeti, naipongeza Kamati hii ikiongozwa na Mhe. Ichung’wah kwa sababu tunapitia nyakati ngumu na tumefanya bajeti hii kwa mazingira ambayo ni magumu sana. Pia, nashukuru Wenyeviti wa Kamati zote za Bunge ambazo zilikuja mbele yetu zikatukabidhi mapendekezo yao. Ulikuwa wakati mgumu lakini tunashukuru kwa sababu tumefika. Nyakati tunazopitia kama nchi ni ngumu. Dunia nzima inapambana na kirusi ambacho, vile wengine wamesema, hatuwezi kukitambua. Kimekuja, tuko nacho na hatujui kitaondoka lini. Wakati wa kufanya bajeti ilitubidi tuangalie kwa makini mapendekezo yaliyotoka katika Hazina kuu ya Kitaifa. Mara ya kwanza, tulipoletewa makadirio na Hazina kuu ya Kitaifa, tuliketi tukakataa mapendekezo yao maanake hawakuwa wameangazia mambo ya kuinua uchumi tena baada ya COVID-19 na hawakuwa wameangazia pesa ambazo zinatakikana ziende kwa idara ya afya ya kuinua hospitali zetu na kuona kwamba tuko tayari kama nchi kupigana na janga la Corona. Tulipokataa mapendekezo yao ya kwanza, ilikuwa ni fursa nzuri kwenda kuketi na kutathmini yale tuliyoyapendekeza. Kwa mfano, tulitaka kujua ndani ya bajeti hii ya kiwango cha Kshs2.7 trilioni ni pesa ngapi zingeenda kupigana na janga hili. Waliporudi, walikuja na Kshs53 bilioni wakatuambia wamezipanga kulingana na vile tuliona inastahili. Mojawapo ya mambo waliyoyasema ni kuwa kuna pesa walitenga kwa kazi mitaani. Ni tumaini la wengi kama Wabunge kazi hizi ziende kwa vijana wetu ambao hawana ajira na zifanywe sawa kwa nchi nzima. Mara ya kwanza ilikuwa ziende kwa miji mikuu. Lakini tunavyojua, hakuna mahali nchini hakujapata shida The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}