GET /api/v0.1/hansard/entries/998556/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 998556,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/998556/?format=api",
"text_counter": 1506,
"type": "speech",
"speaker_name": "Wundanyi, WDM-K",
"speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
"speaker": {
"id": 13509,
"legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
"slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
},
"content": "hii. Kwa hivyo, tunatazamia kwamba kazi mitaani zitaenda kila eneo la wakilishi Bunge ili vijana wetu wapate ajira. Jambo lingine ningetaka kusema sana na ambalo ningetaka liingie katika datari za Bunge ni kuwa raslimali za Kenya mara nyingi zinalenga maeneo fulani. Bajeti hii ina pesa nyingi ambazo zimekadiriwa. Lakini tukiangalia miradi ambayo imewekwa na imetiliwa maanani, kuna sehemu fulani zinapata mgao mkubwa. Kwa mfano, katika sekta ya barabara, mwaka huu nilidhani kwamba maeneo ambayo hayana barabara za lami yangewekwa ndani ya bajeti hii. Aya 16 imetaja Wundanyi kama mojawapo ya maeneo Bunge ambayo hayana barabara ya lami. Kwa sababu ya COVID-19 nilikubali kuwa mwaka huu tutakosa lami. Lakini naomba Bunge hili litilie maanani sehemu ambazo zimebaki nyuma sana kimaendeleo, sana sana katika miundomisingi ya barabara. Jambo ambalo lilinitia kiwewe sana ni kwamba mwaka huu pia nilitarajia mradi wa Mzima II utatengewa pesa. Lakini Waziri alinihakikishia kwamba kwa wiki mbili zijazo, kuna makubaliano yanayoendelea kati ya Wizara na wafadhili kutoka China na kwamba mradi huo utapata ufadhili. Haya ni mambo mazito. Wacha kila sehemu ya Kenya ipate kuwa sawa na nyingine ili kila Mkenya ambaye analipa kodi ajihisi kuwa anafaidika kutoka kwa kodi. Namaliza kwa kusema kwamba ni lazima miundomisingi ya afya izidi kutiliwa mkazo."
}