GET /api/v0.1/hansard/entries/998596/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 998596,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/998596/?format=api",
    "text_counter": 1546,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mwatate, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Andrew Mwadime",
    "speaker": {
        "id": 2451,
        "legal_name": "Andrew Mwadime",
        "slug": "andrew-mwadime"
    },
    "content": " Shukrani Mhe. Spika kwa hii fursa ambayo umenipa. Napongeza Kamati ya Bajeti kwa sababu katika wakati huu mgumu wameweza kuja na Bajeti ambayo tumeona angalao kila idara imepata hela kidogo. Ingawaje tukiangalia, changamoto tuko nazo nchini kama kazi kwa watu wetu. Ukiangalia Idara ya Viwanda, kwa kweli ile hela wamepewa sio eti inawawezesha kutengeneza kampuni nyingi ili vijana wetu wapate kazi. Vile vile, kulikuwa na raha na vifijo na nderemo kule kwangu wakati vijijini umeme ulikuwa unawaka hapa na pale lakini nikiangalia bajeti ya idara ya kawi, naona imepunguziwa hela kidogo. Sioni kama itaendelea tena kuweka umeme kule vijijini."
}