All parliamentary appearances

Entries 91 to 99 of 99.

  • 2 Jul 2013 in National Assembly: Ahsante mhe. Spika. Yangu si mengi kwa sababu nimekaa na Njee Muturi kwa miaka mingi na wana-CORD ambao wako katika Bunge hili walimjua mwaka wa 2001 wakati wa muungano wa NDP na KANU. Njee alikuwa mratibu wetu. Tulitembea na Njee sambamba mpaka dakika ya mwisho. Halafu mwaka wa 2005, wakati wa kura ya maoni ya chungwa na ndizi, Njee alikuwa mratibu wa taifa. Tulimpigia makofi kwa sababu aliweza kutueleza vizuri na tukaenda vizuri na ilikuwa nzuri. Na chama changu cha CORD pia mimi najua ya kwamba kiliendelea vizuri. Yangu si mengi. Nataka kuwaeleze wenzangu ya kwamba hakuna maana tunaita mtu ... view
  • 2 Jul 2013 in National Assembly: Namuunga mkono Njee kwa sababu nambari ya simu alionipatia mwaka wa 2001hajabadilisha. Lakini nasema ya kwamba nina imani na wenzangu. Naunga mkono kama vile wengine wamefanya na hii ni mambo ya nchi yetu ya Kenya. Sio jambo la mtu moja. Nasema kwamba sipingi. Nasema kwamba Njee ako sawa kwa sababu namjua. view
  • 16 May 2013 in National Assembly: Jambo la nidhamu, Mhe. Spika. Kuna mpangilio ambao haueleweki vizuri katika Bunge hili kwa sababu unatoa fursa ya kuzungumza kwa Wabunge wa mrengo wa Jubilee upande huo na upande huu. Baadhi ya Wabunge wa mrengo wa Jubilee wakiona umetoa fursa upande huo, huvuka upande huu ili waweze kupata fursa ya kuzungumza. Tafadhali, lishughulikie suala hili. view
  • 15 May 2013 in National Assembly: Ahsante, Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa hii nafasi. Hakuna mtu aliye na taabu zaidi ya mchungaji. Hawa watu hawavai viatu wala nguo nzuri. Juzi tulikuwa na mkutano mkubwa ambao ulihudhuriwa na Wabunge wa Samburu ya Magharibi, Igembe ya Kati, na Igembe ya Kusini. Mkutano huo ulikuwa juu ya mifugo. Wananchi wanateseka sana wakati wa kiangazi kwa sababu mifugo hawapati maji. Kila mtu analia kwamba hakuna maziwa na nyama. Wakati wa kiangazi anayefuga hawa wanyama huzidi kutaabika. Serikali ya Jubilee siyo mbaya; ni Serikali nzuri. Watu wetu wa CORD ni lazima tusikizane nao. Ni lazima tupendane katika Bunge hili ... view

  • 15 May 2013 in National Assembly: Sisi lazima tuwe pamoja, tupendane na tusikilizane. Zamani kulikuwa na cattle dip ambazo zilikuwa zimejengwa na Moi. Cattle dip zingerudi, lingekuwa jambo la maana sana. Mimi nafurahia kuwa na Jubilee na CORD. Ahsante. view

  • 23 Apr 2013 in National Assembly: Mhe. Spika, mimi ni Mheshimiwa aliyeshindwa mara saba na ya nane akachaguliwa kuja hapa ndani. Natoa shukrani kubwa sana kwa wewe kupata hicho kiti. Najua wewe ni kiongozi ambaye atatuongoza tukiwa pamoja. Natoa pia shukrani kwa Mwenyezi Mungu kunileta hapa na watu wa Tigania Mashariki. Pia nimekutana na ndugu yangu Mhe. Kabando wa Kabando tuliyekuwa naye 1992 na Mhe. Chris Bichage ambaye pia tulikuwa naye tukipigania haki. Kutoka wakati huo, sijawahi kupumzika hadi sasa niko Bunge. Kwa hivyo, nasema ahsante kwa Mwenyezi Mungu na kwa watu wa Tigania Mashariki kwa kunileta Bungeni. Hotuba ya Rais ilikuwa nzuri sana. Sisi watu ... view
  • 23 Apr 2013 in National Assembly: . Naomba Serikali inayoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta na Bw. Ruto - kwa sababu wako pamoja - waunganishe watu wa Tigania Mashariki ili waweze kupanda kahawa. Kahawa ilisaidia sana kuimarisha elimu katika eneo la Tigania Mashariki. Mhe. Spika, Jumapili, nilitembea katika Mkoa wa Kati na rafiki yangu mmoja hapa ambaye sitaki kumtaja. Tulienda kanisani na yeye na akaniuliza: “Mhe. Aburi, nitatoa nini?” Na mimi nikamuuliza: “Kwa nini unaniuliza hivyo?” Akajibu: “Mshahara view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus