All parliamentary appearances

Entries 81 to 90 of 99.

  • 31 Jul 2013 in National Assembly: Asante sana Bw. Naibu Spika wa Muda. Ninaunga mkono Hoja hii. Ninakumbuka kwamba wakati wa Kibaki aliweka pesa nyingi sana katika Banki ya Equity ili zisaidie vijana. Si vijana wote walifaidika kutokana na zile pesa. Kwa mfano, katika jamii ya Wameru, wakati wa vita baada ya kura za mwaka wa 2007/2008, mabasi yalibeba vijana kutoka Eldoret wakamwagwa huko Meru katika mji wa Kolomone. Waliletwa na basi zaidi ya tano. Asubuhi yake waliamkia kwenda kwa Banki ya Equity pale Makutano na tawi lingine karibu na Msikiti Mjini Meru. Kila mmoja wa wale vijana alipata Kshs50,000, ambazo walitumia kununua bidhaa za uchuuzi. ... view
  • 11 Jul 2013 in National Assembly: Asante sana mhe. Spika. Nilikuwa nafikiria kwamba ni jamii ya Wameru tu imeumia. Hiki ni kitu cha kushitua sana. Ukweli wa mambo ni kwamba, mwaka wa 2018 hakuna Mheshimiwa atarudi hapa. Ikiendelea vile ilivyo, hata Rais wetu, Uhuru Kenyatta, hapati kura. Ni kwa nini? Juzi nilisikia sauti kwa kipasa sauti ikisema, “Mhe. Rais, karibu Rais wetu mpendwa”. Nikashituka na nikajiuliza: “Kwani Uhuru amekuja kwangu bila kunijulisha?” Mhe. Spika, kama nitakuita Rais, Uhuru Muigai Kenyatta akija kwangu, nitamwita nani? Ninaomba, kama inawezekana, kwa sababu Bunge ndio ngao ya nchi yetu, hayo mamlaka ya gavana ni kama side mirror. Tutasema tuendeshe gari ... view
  • 11 Jul 2013 in National Assembly: Wakati Wambunge walisimama kuomba kura, kama Kabando wa Kabando alienda kule akasema “mkinichagua, nitawaletea maji, nitatengeneza barabara, ile mali ambayo imevunja akina mama mgongo nitaleta hapa, ile hospitali ambayo haina dawa na ile zahanati nitaleta hapa--- view
  • 4 Jul 2013 in National Assembly: Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda. Historia ya miraa ni ndefu sana. Katika mwaka wa 1814, kulingana na historia ya jamii ya Wameru, miraa iliponya mzee mmoja, Bw. Laibuta, aliyekuwa na ugongjwa wa kifua kikuu wakati kulikuwa hakuna hospitali Meru. Watu waliona kuwa huyo mzee angekufa lakini wazee walichemshia view
  • 4 Jul 2013 in National Assembly: na wakaitengeneza ikawa maji maji. Walimpatia huyo mzee hayo maji ya miraa kwa wiki moja na akapona na kuishi maisha mema tangu wakati huo. Ninaunga mkono Hoja hii kwa sababu katika jamii ya Wameru, ukitaka kumleta bibi nyumbani ni lazima uwe na miraa . Bila miraa, huwezi kumleta bibi nyumbani. view
  • 4 Jul 2013 in National Assembly: ni kitu cha maana sana kwa Wameru. Tukizozana au ukosane na mzee wa rika yako ama mama, unaletewa miraa na wazee ambayo imetemewa mate ndio uile na kusema kwamba wewe hukutenda mambo ambayo unawekelewa. Zamani hakukuwa na koti; koti ilikuwa ni ya wazee wa Njuri Ncheke. Wazee wa Njuri Ncheke wakisema kuwa view
  • 4 Jul 2013 in National Assembly: Na simiti pamoja. Bwana Naibu Spika wa Muda kama alivyosema mhe Kajuju, Wameru wanategemea miraa kwa kiwango kikubwa. Wameru wanapokea zaidi ya Ksh20 million kila siku pale Muringene. Miraa nyingine ipo pale Tigania East, mahali panaitwa Mlango. Hizo ni pesa nyingi na ndizo zinatumika kusomesha watoto. Hatuna mahali pengine pa kupata pesa. Sisi Wameru hatuna kitu kingine cha kutegemea ila kilimo cha view
  • 4 Jul 2013 in National Assembly: Tunataka kilimo cha miraa kiwe sawa na kilimo cha mahindi, majani chai, kahawa ama ndizi. Hii ni kwa sababu miraa ni chakula kama vyakula vingine. Watu waliompigia mhe Wanjohi kura kule Mathare ni wafanyi biashara wa view
  • 4 Jul 2013 in National Assembly: ; walikuwa watu zaidi ya asilimia 80. view
  • 4 Jul 2013 in National Assembly: Pesa zinazoingia katika jimbo la Meru kutoka kwa mhe Wanjohi ni nyingi mno. Mimi naunga mkono kwamba biashara ya miraa iendelee. Wakati wa vita kule Turbo, Eldoret, na Molo mwaka wa 2007 mlisoma kwenye magazeti kwamba watu waliobebwa na mabasi ya Eldoret Express walimwagwa pale Gakoromone sokoni. Waliingia katika benki ya Equity na wakapewa kila mtu Ksh50,000. Vijana wetu Wameru waliokuwa wakifanya hawking walipewa pesa wakanunua nguo na bidhaa nyingine ili wafanye biashara. Je, mkipiga miraa marufuku na hali kazi ya hawking miraa ilifungwa, view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus