Simon Nganga Kingara

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 21 to 30 of 175.

  • 13 May 2021 in National Assembly: Hon. Chairman, I beg to move that the Land (Amendment) Bill (National Assembly Bill No. 54 of 2019) be now read the Third Time. I also request Hon. Waihenya Ndirangu, Member for Roysambu, to second. view
  • 6 May 2021 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia mwanya huu ingawaje tumengojea sana. Kwanza kabisa, naunga mkono Mswada huu ulio mbele yetu. Ni vizuri kuwakumbusha Wabunge wenzangu kuwa wakati tulichaguliwa kwa Bunge, tuliangalia wale Wabunge wako na idadi kubwa sana ya wafuasi na nikapata kuwa ni Wabunge 80 peke yake ambao wana watu wengi katika Bunge hili. Wakati tulienda kwa Spika kujaribu kuangalia vile tunaweza kuwa na usawa, tulikuwa na changamoto kupata nafasi. Kwa hivyo, wakati tumepata nafasi ya kuhusishwa na kusema mapendekezo yetu, nimeona ni jambo la busara sana. view
  • 6 May 2021 in National Assembly: Ukiangalia Mswada huu na yale marekebisho yako mbele yetu, moja ya muhimu, isipokuwa inakuja kwa pole pole, ni kuwa Mswada huu unataka tuwe na uwuiano kwa Afrika Mashariki na hasaa Afrika kwa jumla. Pia ni pendekezo la Mheshimiwa Suluhu wakati alikuja hapa. Aliongea vile tunaweza kuwa na usawa na maendeleo lakini maendeleo hayawezi kupatikana kama hakuna uhuru na suluhu ya maendeleo yale. Jambo moja la kufanya kutafuta suluhu ya maendeleo yale ni kuwa na usawa katika usambazaji wa rasilimali ya Serikali na vile vile usawa katika mambo ya kazi za mashinani hasaa maeneo Bunge. view
  • 6 May 2021 in National Assembly: Nikigusia jambo hilo, ningetaka kutambua kuwa Eneo Bunge la Ruiru ambalo ninawakilisha saa hii liko na idadi ya watu 600,000. Mwaka wa 2019, eneo Bunge hilo lilikuwa na watu 490,000 na eneo Bunge hilo liko na watu wengi kuliko zaidi ya kaunti sita ambazo nitataja. Hata hivyo, mapato huwa ninapewa kama Mbunge wa eneo Bunge linguine. Kaunti ya Samburu ina watu 300,000. Kaunti ya Tana River ina watu 300,000. Kaunti ya Taita Taveta ina watu 340,000. Kaunti ya Tharaka-Nithi ina watu 393,000 na Kaunti ya Lamu ina watu 140,000, lakini Ruiru ambalo ni eneo Bunge, lina watu 490,000. Hata hivyo, ... view
  • 6 May 2021 in National Assembly: Mtu mwingine anasema eti ninadanganya. Nataka watu wapitie mastakabadhi hayo na watapata kuwa ninachosema ni kweli kabisa. view
  • 6 May 2021 in National Assembly: Saa hii nikisimama hapa nikichangia, wale watu wanataka bursary kwangu, wale ambao wamekuja kuomba bursary kwangu kutoka Eneo Bunge la Ruiru, ni watu 90,000. Watu 90,000 wameleta fomu kwenye meza yangu lakini pesa ambazo niko nazo ni Ksh30 milioni peke yake. Ukigawa pesa hizo, kila mtu atapata Ksh333 peke yake. Ninawakilisha nani? Usawa uko wapi katika usambazaji wa rasilimali ya Serikali? The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 6 May 2021 in National Assembly: Kwa hivyo, ombi langu ni kuwa watu wakumbuke jinsi watu kama King’ara wanakaa kule na watu hao. Haitawezekana kuwa na maendeleo mwafaka katika Eneo Bunge la Ruiru na maeneo mengine yalio na watu wengi kama hakuna usawa katika usambazaji wa rasilimali ya Serikali. view
  • 6 May 2021 in National Assembly: Jambo lingine ningependa kugusia ambalo linaweza kuleta maendeleo mema ni kama mawaziri watatoka katika Bunge. Mawaziri wakitoka katika Bunge, pesa za Serikali hazitatumika sana kwa sababu wengi watakuwa wamechaguliwa kutoka Bunge. Lakini changamoto ni vile imeandikwa pale eti “labda wanaweza”. Ningeomba ikiwa inaweza kuwa lazima watoke katika Bunge. Ikiwa hivyo, hata ule uoga haungekuwa na sisi. view
  • 6 May 2021 in National Assembly: Jambo lingine ningegusia linahusu usawa wa Independent Electoral and Boundary Commission (IEBC). Ukiangalia katika utaratibu na pendekezo la IEBC, Mbunge mmoja anatakiwa kusimamia watu 133,000. Kwa hivyo, wakati unapopata suluhu ya kugawa Ruiru kwa vipande kama vitatu ili niache kuwakilisha watu 600,000 ili niwakilishe watu 160,000, ingekuwa sawa. Kwa hivyo, sioni ni kwa nini watu hawaoni haja ya kuunga mkono Mswada huu. Vilevile, ukiangalia kama sasa na watu wako wengi namna ile na rasilimali ni kidogo, hospitali, shule, usalama na pesa za barabara ni duni halafu tunalalamika na sisi ndio tumekataa kuweka mikakati mwafaka itakayoweza kuleta uwiano katika maendeleo ya ... view
  • 6 May 2021 in National Assembly: Kwa unyenyekevu, muda wangu umeliwa kidogo. Naomba dakika mbili niweze kutamatisha. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus