GET /api/v0.1/hansard/entries/112249/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 112249,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/112249/?format=api",
"text_counter": 306,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Sisi tumekuwa katika hoja kama hii wakati ule wa mwisho wa kutafuta Katiba. Tulikaa hapa mpaka usiku wa manane, lakini tulikuwa tunapigana; tulikuwa hatufanyi maridhiano. Kwa wakati huu, Wakenya wameamua ya kwamba lazima tupate Katiba. Na sisi Wabunge tumeamua kwamba, hata watuambie nini huko nje; watuseme, watuandike, watufanyeje, watutukane--- Wengine wanasema--- Eti leo katika gazeti moja ambalo Mbunge amezungumzia hapa---Gazeti limesema tunakataa kupitisha Katiba kwa sababu tunangoja ridhaa. Ni haki gani kuzungumza mambo kama hayo; kuleta madharau kwa Bunge letu? Wakati unaandika mambo hayo, ndio gazeti lako litanunuliwa na tutakupigia makofi lakini, kumbuka ukivunja hadhi na heshima ya Bunge, unajiumiza wewe kama Mkenya wa kawaida."
}