GET /api/v0.1/hansard/entries/1222992/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1222992,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1222992/?format=api",
    "text_counter": 91,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nyali, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Mohammed Ali",
    "speaker": null,
    "content": "Kisha angalia vijikike viwili vimesimama kando ya barabara vikifanya vile vile. Siku hizi hawana hata haya; hawana aibu. Wanachapisha vitabu na kuweka picha zao mitandaoni wakisema, “ I am in love”. Lo! I am in love kiatu changu! Hatutakubali tabia hiyo sisi kama Wabunge. Hatutaikubali kama nchi. Hii nchi ina Mungu na ina dini."
}