GET /api/v0.1/hansard/entries/1625485/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1625485,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625485/?format=api",
"text_counter": 236,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ibara ya 37 ya Katiba ya Kenya inakubali maandamano ya amani. Inavunja moyo sana ukiona watu wanaandamana wengine kwa amani ilhali kuna wahuni. Jambo la kuvunja moyo zaidi ukitembea Nanyuki – kwa sababu kulikuwa na maandamano ya Saba Saba - msichana wa miaka 24 ambaye ni Julia Njoki alishikwa, akapelekwa kortini na kuhukumiwa. Kwa njia isiyojulikana alifia katika seli."
}