GET /api/v0.1/hansard/entries/7643/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 7643,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/7643/?format=api",
"text_counter": 306,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Ethuro",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 158,
"legal_name": "Ekwee David Ethuro",
"slug": "ekwee-ethuro"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa kumshukuru Waziri kwa Kiswahili sanifu. Waziri amesema kuwa barabara kutoka Kachibora hadi Sibanga inaelekea Kitale. Ningependa kumkumbusha Waziri kwamba, - inafaa ajue - barabara kutoka Kachibora mpaka Sibanga inapitia Makutano, Kapenguria mpaka Lodwar. Kwa vile amesema atatengeneza barabara hizo zote, je, atarekebisha lini barabara ya Sibanga- Makutano-Kapenguria-Lodwar? Ametenga pesa ngapi za kurekebisha barabara hii ili nami nimwalike Rais aje aifungue barabara hiyo?"
}