25 Nov 2024 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii nami niweze kupenyeza sauti yangu kwa kuichangia Hotuba ya Rais aliyokuja kuzungumza hapa, kwa taifa.
view
25 Nov 2024 in National Assembly:
Kwanza, nizungumzie swala la Adani. Kwa kuivunjilia mbali kandarasi ya Adani, Mhe. Rais amefurahisha Wakenya wengi kwa sababu ni jambo ambalo lilikua limeleta utata mkubwa. Wafanyikazi wote walikuwa na wasiwasi kwamba badala ya kulipwa kwa mwezi, watabadilishwa kuwa na mikataba. Ni jambo la utata mkubwa kuona rasilimali yetu tunayoitegemea, mtu akikuja kuisimamia kwa miaka 30. Kwa hivyo, ilikua ni wasiwasi mkubwa. Alipoifutilia mbali, amefanya jambo nzuri. Amesikiliza wananchi, na kiongozi yeyote ni yule anayesikiliza wananchi. Kwa hivyo, hilo nampongeza Mhe. Rais.
view
25 Nov 2024 in National Assembly:
Nikija katika upande wa shilingi kuwa na nguvu, ni kweli, shilingi yetu ilikuwa imekosa thamani kubwa. Hata ilikuwa ukienda kwa nchi jirani kubadilisha pesa yetu ya Kenya wanaikataa. Wanasema pesa ya Kenya haieleweki kwa maana leo iko hivi, kesho iko chini zaidi. Lakini imeimarishwa na mpaka sasa pesa yetu inaheshimika. Kushuka kwa dola, sisi tunategemea kwamba taifa litaimarika wakati pesa za kigeni na hali ya uchumi kama mafuta yataweza kushuka bei. Isipande kwa sababu dola imeanguka. Kwa hivyo, wananchi wanategemea wakati dola imeendelea vizuri na pesa zitashuka ili kusudi mwananchi aweze kujikimu ama gharama za maisha zisiweze kupanda juu.
view
25 Nov 2024 in National Assembly:
Tuje katika upande wa SHA. Mimi mwenyewe nimeweza kushuhudia wagonjwa wa moyo katika Hospitali ya Rufaa ya Mombasa, yaani Coast General Hospital . Kuna mgonjwa ambaye alienda kuwekewa pacemaker au kifaa ambacho kinaweza kufanya moyo wake upige kwa usawa, bill yake ikaja Ksh1.3 milioni. Na nikashangaa kuona SHA imemlipia Ksh1.1 milioni papo hapo. Kwa hivyo, nimeona ni jambo ambalo kama watalitilia bidii; kama hawatabadilika, hii SHA itasaidia sana mwananchi wa kawaida. Na vile vile, ukiangalia SHA katika levels 2, 3, 4 hospitals, ukipiga tu kwenye simu yako *147# ili kujisajili, wewe unatibiwa bila malipo. Ikiwa itaendelezwa vile inavyoendelea sasa, itawasaidia ...
view
25 Nov 2024 in National Assembly:
Hivi sasa, SHA kwa mwezi ni shilingi Ksh300, NHIF ilikuwa Ksh500. Kwa hivyo SHA kwa mwaka ni Ksh3,600. Nina imani kwamba ikiwa watajipanga vizuri, itakuwa jambo la busara kwa sababu matibabu ni ghali sana na mwananchi wa kawaida hawezi kulipa. Katika NHIF, kulikuwa na uzito mmoja. Wakati unaambiwa unangoja approval, unaweza kungoja masaa matatu au matano kabla kupewa hiyo ruhusa ya kupewa dawa ama kuruhusiwa kwenda nyumbani. Lakini SHA kwa sasa ni kwamba ukingoja approval, hauchukui muda. Kwa hivyo, ikiwa wataendelea namna hii, basi itasaidia wananchi sana. Juzi tu nimetembelea hiyo hospitali na SHA wamelipa kufikia sasa Ksh21.9 milioni kwa ...
view
25 Nov 2024 in National Assembly:
Tukienda kwa upande wa chakula, bei za chakula zimeshuka. Unga zamani ilikuwa inanunuliwa kwa Ksh160. Mhe Rais alisema ukweli kuwa bei ya unga imeshuka lakini shida iliyoko ni kwamba uchumi wa taifa unaimarika ikiwa pesa imeingia katika mifuko ya wananchi. Ikiwa wananchi wana fedha, basi uchumi huwa mzuri. Lakini kama mwananchi hana fedha, uchumi utakuwa wa kuzungumziwa tu. Mwananchi hatakuwa na faida.
view
25 Nov 2024 in National Assembly:
Nikimalizia, kwa sababu muda wangu naona umekwisha, ningependa kuzungumzia kazi katika mataifa ya nje. Kweli, zimekuja juzi na zimesaidia watoto wengi. Lkini kuna watu ambao…
view
25 Nov 2024 in National Assembly:
The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
25 Nov 2024 in National Assembly:
Naomba dakika moja.
view
25 Nov 2024 in National Assembly:
Kwa hivyo, vijana wapelekewe kazi kule waliko ili ziwasaidie. Ama watu watasema kwamba zile kazi zimekuja kwa ubaguzi. Kwa hivyo, kazi zingine kule Ujerumani, Uajemi ama nchi zingine zikija, zote zigawanywe katika maeneo yote, ili kila mmoja aweze kufaulu. Kwa haya mengi…
view