Bady Twalib Bady

Parties & Coalitions

Born

1st May 1974

Email

badibadi94@yahoo.com

Telephone

0722346475

All parliamentary appearances

Entries 1 to 10 of 177.

  • 2 Feb 2022 in National Assembly: Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwanza, nataka kumpongeza Mhe. Barasa kwa kuja na Mswada huu. Pia, tumeona kuwa watu wengi wanafanya kazi na baadaye, wanaishi katika ufukara. Vilevile, wengine wanakufa kabla ya kupata marupurupu yao. Mhe. Barasa amefanya vizuri katika Mswada huu kwa kuwa yatakikana mtu akifika kustaafu, kabla hata hiyo miezi mitatu haijafika ndio aanze ile mipangilio ya kufuatilia hii pesa, ni muhimu Serikali ishughulikie mambo haya ili mtu anapostaafu, anapewa pesa na malimbikizi yake yale anayostahili kupewa mara moja. Pia, tuanona kuwa kumefanyika ugatuzi kwa mambo mengi. Kwa hivyo, kwenye marupurupu, ingekuwa bora zaidi pia badala ... view
  • 2 Feb 2022 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii. view
  • 2 Feb 2022 in National Assembly: Kwa niaba yangu, kwa niaba ya familia yangu na kwa niaba ya wananchi wangu wa Jomvu, natuma rambirambi zetu kwa wale waliopata mkasa wa moto kule Mvita. Pia mimi binafsi, natuma pole kwa ndugu yangu, Abdullswamad Sheriff Nassir, Mbunge wa Mvita. view
  • 2 Feb 2022 in National Assembly: Tunaunga mkono Mswada huu kikamilifu kwa sababu wahudumu wa afya wa jamii wako katika sehemu zetu na wanafanya kazi kubwa sana. Ni wakati hivi sasa Serikali ya Kenya kutengea wahudumu wa afya wa jamii bajeti yao na wawekwe motisha kwa kazi nzuri wanayoifanya. Watu hawa hawalipwi. Naweza kutoa mfano kutoka eneo langu la Jomvu, ambapo kuna hospitali Miritini, na wengi wanaofanya kazi huko ni wahudumu wa afya wa jamii. Wanaofanya kazi wengi katika Jomvu Model Hospital ni wahudumu wa afya wa jamii. Mikindani pia, wanaofanya kazi ni wahudumu wa afya wa jamii. The electronic version of the Official Hansard Report ... view
  • 2 Feb 2022 in National Assembly: Kukitokea jambo lolote, mkasa ama jambo kama lile lilitokea pale Mvita, wahudumu hawa ndio watu wa kwanza tunawaona wanakimbia kuokoa maisha ya wananchi. Vile vile kama tunavyoelezwa na jina lenyewe, wako kabisa mashinani kwa jamii. Wanatembea hata wakati tumekumbwa na ugonjwa wa Corona. Wanashikana na machifu, wazee wa mitaa na wengine wengi sana kuangalia matatizo yanayopatikana kwa watu. Wanakimbia katika vijiji lakini hawalipwi, hawapewi motisha, na hawapewi nguvu yoyote. Wanafanya kazi katika hali ngumu sana kwa sababu hawana vifaa, na vile vile wakati wa kuwapatia taluuma ya kuangalia vile wataweza kuondoa shida zilizoko katika sehemu zetu, inakuwa ni shida. Wanafanya ... view
  • 2 Feb 2022 in National Assembly: Kama wenzetu walivoyosema, ni wakati mwafaka hivi sasa kuona kwamba bajeti ya Kenya inatenga pesa za kuwasaidia wahudumu wa afya wa jamii. Nataka kubatiliza katika Mswada huu ili kuzungumuzia wengine kidogo. Sio wahudumu wa afya wa jamii pekee yake. Hata mabalozi, wazee wa mitaa wanafanya kazi kubwa, lakini tukiangalia chifu na mkuu wa tarafa, wanaonekana wamefanya kazi kumbe imefanywa na wazee wa mtaa na balozi ambaye yuko pale. Kwa hivyo, ni muhimu kuona kuwa watu kama hawa wanaofanya kazi nyanjani wanapewa motisha na pesa. Pesa nyingi zinapotea nchini. Zinapotea kwa sababu ya ubadhirifu wa pesa unaoonekana. Ubadhirifu wa pesa ulionekana ... view
  • 2 Feb 2022 in National Assembly: Nachukua fursa hii kusema kuwa nimeona hali hii kwa sababu nilikuwa diwani kutoka mwaka wa 2007 mpaka leo nimekuwa kiongozi katika sehemu yangu. Haya matatizo ndio tunaambiwa kila siku katika sehemu zetu. Hivi sasa katika Bunge hili, tunataka tuweke rekodi kuwa jambo hili tulichangia, na Serikali ikalitia maanani kuona pesa zimepatika ili watu hawa waweze kusaidiwa. view
  • 2 Feb 2022 in National Assembly: Nachukua fursa hii pia kumpongeza Mhe. ndugu yangu aliyeleta Mswada huu wa maana sana kwa sababu utasaidia maelfu ya watu ambao wanafanya kazi katika nchi hii nzima kwa kuhakikisha kwamba watawekwa katika hesabu ya manufaa ya kuhudumu nchini. view
  • 2 Feb 2022 in National Assembly: Kwa hayo ambayo nimeongea, kwa sababu ya muda, nakomea hapo. Shukrani kwa kunipa nafasi na nawachia hapo ili wenzangu waweze kuchangia jambo hili. Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. view
  • 10 Nov 2021 in National Assembly: Thank you, Hon. Deputy Speaker. I rise to ask Question No. 467/2021 to the Cabinet Secretary for Lands: (i) Could the Cabinet Secretary explain the reasons behind the sudden blockage of Maganda Road, CR.68111, in Jomvu Constituency despite the road having served the public for over 60 years? (ii) Under what circumstances has the blockage been undertaken and a wall erected, notwithstanding the fact that the road lies on public land L.R. No. 3851/VI/MN? (iii) Within what timelines shall the erected wall be demolished and the road restored to enable the residents obtain critical access to schools, hospitals, government offices ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus