23 Apr 2024 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view
23 Apr 2024 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, ni aibu sana kwa sababu kama Kaunti ya Nandi, tunajivunia kuwa na wanariadha na hatuna uwanja wa kimataifa. Kama ujuavyo, wanariadha waliobobea, Bw. Eliud Kipchoge na Bw. Kipchoge Keino wanatoka katika Kaunti ya Nandi. Bw. Henry Rono ambaye tulimuzika majuzi na tunaendelea kuiombea familia, pia anatoka katika Kaunti ya Nandi. Pamela Jelimo na Janet Jepkosgei ambaye watu wengi wamempa jina la utani, Eldoret Express, pia wanatoka katika Kaunti ya Nandi. Hata hivyo, ni aibu kwa Kaunti ya Nandi na serikali za ugatuzi kwa sababu zimezembea. Wameshindwa hata kujenga kiwanja cha mbuzi ambako wanaweza fanya mazoezi. Mimi ...
view
23 Apr 2024 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, niko na sheria ambayo najaribu kuongeza asilimia ambayo inaenda katika kaunti, kutoka asilimia 15 mpaka 40. Ni aibu sana kuwa bilioni za pesa zimeenda katika Kaunti ya Nandi. Hata hivyo, Gavana wangu alipata muhula wa pili. Akiwa kule mashinani, alisema kwamba yeye hakushinda lakini alitumia mpira wa mkono ili apate muhula wa pili. Hiyo ndiyo sababu hatujaweza kuona maendeleo yeyote, hasa katika Kaunti ya Nandi. Nimeona Maseneta kama vile Sen. Abass na viongozi wa Walio Wengi na Walio Wachache Bungeni wakitaja Nandi. Kiongozi wa Walio Wachache amesema Nandi imejaa wanariadha. Lakini, hatuna viwanja vya michezo ambazo ...
view
23 Apr 2024 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view
23 Apr 2024 in Senate:
kupewa nafasi ya kushiriki katika hilo dimba la mpira ambalo. Ni lazima tuwe tayari ikiwa dimba hilo litafulu. Bw. Spika wa Muda, mara nyingi Naibu wa Rais, Mhe. Rigathi Gachagua anapambana na mambo ya madawa ya kulevya na miharadati katika taifa letu la Kenya. Tukitaka kuangamiza janga hilo ni lazima tuhakikishe viwanja na kumbi za michezo zimetengenezwa ili vijana wapate mahali pakupata uraibu wa michezo mbalimbali katika taifa letu la Kenya. Nilikuwa na hoja tatu. Tunapoelekea katika michezo ya Olimpiki mwaka huu kule Paris, Ufaransa, nataka kuwaomba Wakenya tupeane ufadhili ambao tukonao ili kuhakikisha wanariadha ambao wanaelekea huko wamepata ufadhili ...
view
23 Apr 2024 in Senate:
Ninakupata, Bw. Spika wa Muda. Hata hivyo, ukiangalia katika sehemu ya Katiba 96, Bunge la Seneti liko na jukumu la kuchunga na kulinda mambo ya ugatuzi. Bw. Spika wa Muda, ingawa na zingatia onyo lako, tukiona ugatuzi unaangamizwa katika kaunti yoyote, kama Bunge ni vyema kuitaja ndio kupitia ofisi yako na ya Seneta wa Kaunti ya Narok afuatilie. Hii ni kwa sababu tumepigania haki ya demokrasia katika ----
view
23 Apr 2024 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, ninakubaliana na wewe. Lakini kupitia ofisi yako na kiti chako, kwa heshima kubwa, ni muhimu Seneta wa Narok na Bunge hili walivalie njuga suala hilo, hasa Kamati ya masuala ya Ugatuzi ndio tuweze kujua kinacho endelea kule katika Kaunti ya Narok. Kwa heshima, naunga mkono Hoja hii. Tuko na jukumu kama taifa. Kenya inajulikana sana kwa kubobea kwa wanamchezo na wanariadha ambao wametajika. Nataka kumuunga mkono Seneta wa Mombasa kwa hii Hoja. Asante, Bw. Spika wa Muda.
view
23 Apr 2024 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, ningependa kumweleza ndugu yangu kiongozi ambaye anapambana na “Bullfighter” kuwa kama Naibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Pesa za Umma, niliongoza jeshi la Maseneta kuzuru Kaunti ya Mombasa. Tulipofika huko, tulipata kuwa ule uwanja wa michezo ulikuwa umebadilika na kuwa mahali pa wanyama kuishi. Kuna “majisimba” na “majizimu” katika uwanja huo ilihali, katika bajeti na hesabu za ukaguzi, kuna zile stakabadhi zote za kuonyesha kwamba, wakati Mhe. Joho alikuwa Gavana katika kaunti ya Mombasa, aliweka zaidi ya shilingi milioni mia tano.
view