12 Oct 2021 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili nizungumze machache kuhusiana na taarifa ambayo imeletwa na Sen. Dullo. Kwanza, nataka kumpongeza kwa kuleta taarifa hii kwa wakati huu. Huu ni wakati mwafaka na imekuja wakati ambao unafaa. Unapozungumza mwisho huwa mengi yamezungumzwa lakini kuna mengine ambayo nitasisitiza. Inasemekana kuwa kitambulisho ni haki ya kila mtu, nami pia naamini hivyo. Kuna masuala ambayo yanazungumziwa ambayo nitayazungumzia, kuhusu usajili wa vitambulisho. Wakati mtu anasajiliwa ama ameenda kusajiliwa, yale maswali yanaoulizwa yanaudhi. Wakati mwingine wale ambao wanahusika kwa usajili wanaandika majina yakiwa na makosa ambayo yanaleta shida baadaye. Kwa mfano, mamangu ...
view
12 Oct 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
12 Oct 2021 in Senate:
zamani na nikaambiwa nikatafute cheti chake cha kuzaliwa ambapo hakuwa nayo. Mimi sikuwa na cheti hiyo na hata yeye hakuwa nayo. Hii ndio maana nikawa nimeenda kutafuta cheti cha kuzaliwa kwa sababu nilikuwa nataka kupata pasipoti niliambiwa ni lazima niwe nayo. Kwenda pale nikaambiwa nipeleke cheti ya kuzaliwa ya mamangu na alikufa zamani na alikuwa hana cheti hiyo. Nitaipata wapi? Baadaye nikaambiwa nitafute kitambulisho chake, sijui kilipotea vipi kwa kuwa mamangu alikufa kitambo nikiwa mtoto mdogo. Nikaenda kwa chifu kwa kuwa tunajuana na yeye - naenda hapo kwa sababu amezungumzia Sen. Omogeni kuhusu machifu - aliandika barua kwamba mamangu ni ...
view
12 Oct 2021 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, kuna huu ugonjwa wa UKIMWI ambao ulikuja. Watoto wengi wameishi hawana wazazi, kabla dawa za kuua UKIMWI ndio uishi kwa siku nyingi, watu wengi walikufa wakati ule. Watoto wengi ni mayatima, wanaishi na nyanya zao ambao walikuwa wazee na pengine walikufa. Ukienda kumuuliza maswali mtoto kama huyu hajui akwambie nini, mamake, babake na nyanyake hakumuona. Tukitaka taarifa ya huyu ni tujue kwa mzee wa kijiji ama mzee wa nyumba kumi ambaye ana taarifa ya mtoto alipozaliwa. Hospitalini kazi imekuwa rahisi. Kwa sababu watoto wangu wote nimewazalia hospitali naezaenda na kuuliza stakadhabi zake zote za mtoto wangu ...
view
12 Oct 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
12 Oct 2021 in Senate:
Haya maswali mtakayouliza muulize maswali ya hadhi na mtoto hatajihisi kwamba amebaguliwa na kutengwa katika jamii. Naunga mkono Statement ambayo imeletwa na kuna zile hatua ambazo zinafaa kuchukuliwa ili watu watajitokeza kwa wingi na kuchukua vitambulisho. Nasihi Kenya nzima na Kaunti ya Kilifi ambako natoka, kuna wakati kulikuja Mswada hapa Bunge, ni vile haukupita, kwamba shilingi moja, mtu moja, one man one vote one shilling. Bw. Spika wa Muda, kusema kweli, kama Mswada huo ungepita, sisi watu wa Kilifi tungekuwa na shida sana. Hii ni kwa sababu tuko wengi, lakini wengi bado hawajachukua vitambulisho. Kwa hivyo, inakuwa shida kupiga kura ...
view
7 Oct 2021 in Senate:
Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa niweze kuwakaribisha Wabunge wa Kaunti ama MCAs kutoka Nandi. Ningetaka nikubaliane na wenzangu wengi kwamba katika Maseneta wachangamshi basi mmoja wao ni Seneta wa Nandi. Kusema ukweli, kama ingekuwa kuzungumza pekee yake ndio kunamrudisha mtu hapa Bunge, nina hakika kwamba angerudi hapa Bunge. Hata hivyo, ninaamini kuwa watu wa Nandi wanamuona na wako pamoja na yeye. Vile vile, ningependa kuwaambia MCAs wawe huru. Mnakaribishwa na pia mnaweza kufika hapa. Mimi ninayezungumza hapa, kipindi kilichopita nilikuwa MCA kule Kilifi lakini kwa njia zingine zisizoweza kuepukika nilijipata hapa. Kwa hivyo, hakuna lisilowezekana mbele ya Mungu. Kila ...
view
7 Oct 2021 in Senate:
Asante Bw. Spika. Ninasimama kuunga mkono malalamishi yaliyoletwa kwetu kuhusu mambo ya afya na kadi za hospitali za NHIF. Kusema ukweli, watu walikufa zamani lakini hivi sasa, watu wanakufa zaidi. Wengine hawakufi kwa sababu hawangeweza kupona. Ijapo kuwa Mwenyezi Mungu ndiye huchukua roho, watu wanakufa kwa sababu wanakosa matibabu yanayohitajika kwa wakati unaofaa. Nitapeana mfano wa wagonjwa wa Korona ambalo ni janga la taifa na silo la mtu mmoja, la kujitakia wala kulileta. Lakini, ukipata ugonjwa wa Korona na ufike hospitalini na uwekwe kwa oxygen, uko na shida. Hii ni kwa sababu, ukiwekwa kwa chumba cha hali mahututi, siku mbili ...
view
7 Oct 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
7 Oct 2021 in Senate:
Kwa hivyo, nikitoka hapa, nitafuata Maseneta walio hapa mnisaidie niweze kupata dosi moja alafu ning’ang’ane kupata hizo zingine. Bw. Spika, kwa hivyo, kuna haja ya kadi za hospitali zisimamie hayo magonjwa kwa sababu hatujui unavyokuja na kuingia ndani ya mwili. Mtu hujipata tu ako nao. Kama kadi itasaidia mgonjwa wa Malaria, mimi pekee yangu bila kwenda hospitali naweza ng’ang’ana na mtu akapona. Lakini, saratani ni ugonjwa ambao unahitaji watu wengi wakusanyike mahali pamoja. Taifa la Kenya lichukue jukumu la kuangalia watu wake ambao wanashikwa na yale magonjwa ambayo wanadamu hawawezi kujisimamia. Ninaunga mkono malalamishi hayo kwa dhati na nguvu zangu ...
view