All parliamentary appearances
Entries 1 to 10 of 908.
-
3 Dec 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa nafasi hii ambayo umenipa kuchangia. Mambo ya fedha za uzeeni ambazo wafanyikazi wanatozwa ni jambo nililotaja wiki iliyopita. Hili ni jambo la kusononesha sana. Bunge hili la Seneti limegeuzwa kuwa kinanda mbele ya Wakenya. Haiwezi kuwa leo ni santuri ya fedha za kustaafu, wiki ijayo kama, Bw. Naibu Spika, unaweka santuri ile ile. Sio vyema wala haki kwa Wakenya kutuona sisi kama walalamishi wasio na suluhisho. Naomba tutamatishe shughuli hii kwa kuuliza Serikali ya Kitaifa, watumishi wa umma pesa zao zipo ama hazipo? Viongozi katika kaunti - magavana watuambie, pesa za wafanyikazi zipo ama ...
view
-
3 Dec 2024 in Senate:
Jambo la pili, katika usajili huo, nimeona katika kaunti zetu, fedha za afya,
view
-
3 Dec 2024 in Senate:
ya baadhi ya wafanyikazi hazilipwi. Wanasononeka na kutaabika. Kwangu Bungoma wafanyikazi wanalia. Wakienda hospitalini wanaambiwa Britam haijalipa. Britam haitekelezi wajibu wake. Nami naomba Serikali iamuru kwamba pesa zitolewa ziende katika kaunti.
view
-
3 Dec 2024 in Senate:
Bw. Naibu Spika, ni kitendawili ama ni kinaya, hadi sasa kaunti yangu ya Bungoma pesa hazijafika. Wananiambia yule ambaye anastahili kuweka sahihi ili malipo yafanyike hayupo. Nami naomba anapopatikana, fedha ziende kwa wale ambao wanapaswa kulipwa. Kama ni wanakandarasi walipwe. Watu wasilipwe ilhali mradi unaenda kubadilishwa baada ya mwezi moja. Ni jambo la kustaajabisha kuwa serikali za kaunti zimeanza kucheza shere na Serikali ya Kitaifa hapa Nairobi. Unapata mwezi huu serikali ya kaunti inatoa shilingi 10 milioni kurekebisha muundo msingi fulani na baada ya miezi miwili, serikali ya Kitaifa inaweka pale shilingi 200 milioni. Sasa shilingi 10 milioni ni ya ...
view
-
20 Nov 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Ningependa kuchangia kuhusu macadamia na mimea ambayo hutoa mafuta. Mimi nataraji kwamba Serikali kabla haijaamua ama kukata kauli kuhusiana mmea wowote nchini, lazima washika dau wote wahusishwe katika mchakato mzima. Haiwezekani kwamba Waziri ama viongozi katika Wizara, wataamka asubuhi na mapema kupitisha sheria ambayo inamgandamiza mkulima wa makandamia nchini. Haiwezi kuwa wanakata kauli kuboresha pesa ambazo mabwenyenye wanapata kuliko kuangalia hali ya maisha ya mkulima wa makandamia nchini. Mimi na mwenzangu mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi samawati, hivi karibuni tutamkaribisha mheshimiwa Waziri kuweka bayana kile kilichosababisha kuwanyima wapandaji ama wakulima wa makandamia nafasi ya kupata kipato kwa ...
view
-
20 Nov 2024 in Senate:
Madam Temporary Speaker, what my good doctor and bullfighter said is that we welcome and we will do what we always do to guests and honourable people from our community. On behalf of Bungoma County, I also welcome my mothers in the House. I thank you.
view
-
14 Nov 2024 in Senate:
Thank you, Mr. Speaker, Sir. I request to be protected from the noise.
view
-
14 Nov 2024 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, I rise pursuant to Standing Order No.53(1) to seek a Statement from the Standing Committee on Labour and Social Welfare regarding the status of remittances to the Bungoma County government employees’ pension scheme from 2022 to date. In the Statement, the committee should- (1) State the providers of pension scheme services to employees of Bungoma County Government. (2) Explain whether staff join on voluntary basis or it is mandatory to all employees of the county. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from ...
view
-
14 Nov 2024 in Senate:
(3) Provide a report of all employees covered by the scheme, the amount deducted from their salary per month, and whether the said deductions are remitted to the scheme by the county, stating the number of beneficiaries of the scheme from the year 2022 to date. (4) Provide financial statements showing the remittances of employee contributions by Bungoma County Government for the financial years 2022/2023 and 2023/2024, indicating when the last payment was made. I thank you.
view
-
13 Nov 2024 in Senate:
Asante, Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii angalau kutaja machache kuhusu mchecheto mzima wa mawaziri kukosa kuja hapa kujieleza kwa mapana na marefu. Bibilia inasema kwamba, Yesu alipokuwa anatembea na wafuasi wake, walimuona mwamamke mmoja wakamuita mzinzi na wakataka kumpiga mawe. Yesu kwa busara wake akawauliza ni nani miongoni mwao hana dhambi? Akawaambia yule asiye na dhambi atupe jiwe wa kwanza. Wengi walifyata midomo, wakaweka mikia katikati ya miguu na hatimaye wakamuacha binti huyo aliyekuwa anafanya biashara zake. Mhe. Naibu Spika, hakuna mtu duniani humu hana dosari ama makosa. Kuteleza sio kuanguka. Jumba la Seneti lina haki kikatiba kuwasikiza ...
view